Header Ads

test

MBUNGE SIMA ATAHADHARISHA WAHITIMU UFADHILI WA MASOMO NJE KWA KIGEZO CHA KUUKUBALI USHOGA

 

Wahitimu wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Mwenge  wakiwa kwenye mahafali ya 48 yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Singida.

.........................................................

.Na Dotto Mwaibale, Singida

WAHITIMU wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Mwenge iliyopo Manispaa ya Singida mkoani hapa wametakiwa kuchukua tahadhari kubwa yakutojiingiza kwenye vishawishi vya kupata ufadhili wa masomo nje ya nchi na kujikuta wakiingia kwenye mahusiano ya mapenzi ya jinsia moja kupitia mitandao.

Tahadhari hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Mussa Sima, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 48 ya kidato cha sita katika shule hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki.

  "Sasa hivi zinatumika mbinu mbalimbali na mataifa ya magharibi kama mnavyoona jinsi serikali yetu inavyopambana na masuala ya ushoga na usagaji  wanaweza kutengeneza mbinu ya wewe kuingia katika shughuli hizo za maadili ambayo sisi hatuna hivyo mnapaswa kuwa makini sana mnaweza kuhitaji kupata maisha ya haraka na  mkajikuta mmeingia kwenye vitendo hivyo," alisema Sima.

Alisema Serikali haikubaliani na mambo hayo lakini mitandao ya kijamii imetoa nafasi ya mtu kufanya chochote lakini Serikali yetu kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezuia vitu ambavyo havina maadili na utamaduni wa kitanzania mfano masuala ya ushoga na picha za utupu.

Sima alisema kutokana na kukua kwa teknolojia mtu anaweza akaingia kwenye mitandao ya kijamii na kukutana na viti hivyo vikiwepo kupata hela au ufadhili wa masomo na bila kujua anajiingiza kujaza fomu  kupatiwa ufadhili wa masomo au kazi na kutumiwa fedha na tiketi ya ndege.

Mbunge Sima alisema watu hao wakija na mbinu hizo za kutoa ufadhili wa masomo katika vyuo mbalimbali nje ya nchi walengwa wanatakiwa kutoa taarifa kwa wizara husika ambayo inavijua vyuo vyote hivyo ili kupata uthibitisho badala ya kwenda kimya kimya na kujikuta wakiharibikiwa.

Aidha, Sima aliwataka wazazi na walezi wa wahitimu hao watakapokuwa  nyumbani wakisubiri matokeo yao kuwapa stadi za maisha kwa kuwafundisha  shughuli mbalimbali za nyumbani ikiwemo ujasiriamali, kilimo ama kujihudumia hatua itakayowasaidia kujitambua na kujilinda katika kipindi hicho.

Pia Mbunge Sima alitoa Sh.Milioni 1  kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa chumba maalumu cha kuhifadhi nyaraka mbalimbali na mitihani baada ya Mkuu wa Shule hiyo, Method Njiku kuelezea changamoto ya kutokuwa na chumba hicho.

Awali akitoa taarifa ya shule hiyo Njiku alisema kuwa imeendelea kufanya vizuri na kushika nafasi ya juu katika matokeo ya mitihani ya taifa na kuwa mikakati waliyonayo ni kuondoa kabisa daraja la nne na kubakiwa na daraja la kwanza na la pili.

Njiku alisema siri  ya mafanikio hayo inatokana na kujiweka malengo, mikakati na kuhakikisha inatekelezwa kwa wakati na kuwa miongoni mwa mikakati hiyo ni kufundisha masomo ya ziada na rekebishi, kutoa motisha kwa walimu na wanafunzi wanaofanya vizuri katika masomo, ushirikiano baina ya bodi ya shule, wazazi, wafanyakazi wanafunzi na wadau wengine wa elimu.

Akisoma risala kwa mgeni rasmi Kilanja Mkuu Mstaafu wa Shule hiyo, Makindoya Shaban alielezea changamoto kadhaa kuwa ni pamoja na ukosefu wa uzio jambo ambalo huathiri usalama na wakati mwingine kuchochea utovu wa nidhamu kwa wanafunzi na utoro.

Alitaja changamoto nyingine kuwa ni kukosekana kwa vifaa vya kufundishia somo la kompyuta na kuwafanya kushindwa kupata maarifa, ujuzi na umahiri wa elimu ya kidigitali sambamba na kutokuwa na gari ambalo litawasaidia katika ziara za masomo.

Shaban alisema Shule ya Sekondari Mwenge ni moja ya shule kongwe hapa nchini na kuwa waanzilishi wa shule hiyo ni Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ambao waliikabidhi kwa Serikali mwaka 1967 kama zawadi ya kuunga mkono malengo ya Azimio la Arusha.

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 48 ya kidato cha sita katika shule hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu hao.
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu wakati wa mahafali hayo.
Makamu Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo akizungumza.
Mkuu wa shule hiyo, Method Njiku  akitoa taarifa ya shule hiyo.
Walimu wa shule hiyo na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wazazi na walezi wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wazazi na walezi wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wahitimu wakitoa burudani.
Twisti ikichezwa wakati wa mahafali hayo.
Mhitimu akionesha umahiri wa kugani mashairi katika hafla hiyo.
Viongoi wastaafu wa shule hiyo wakiwajibika.
Burudani ikiendelea katika mahafali hayo.
Na Msanii huyu naye alikuwepo kwenye mahafali hayo
Mmoja wa wazazi akitoa nasaa zake kwenye mahafali hayo.
Nasaha zikiendelea kutolewa na wazazi katika mahafali hayo.

Taswira ya mahafali hayo.
Afisa Elimu  Kata ya Majengo, Mwalimu Nuru Ntandu akizungumza kwenye mahafali hayo.

Burudani ikitolewa.
Burudani zikiendelewa kutolewa.
 

No comments