TMDA YAPIGA MSASA KWA WATOA HUDUMA MKOA WA IRINGA
Felix zelote afisa usajili wa dawa na vifaa tiba ameelezea namna ya kufikisha matukio
Afisa wa mamlaka ya udhibiti wa dawa na vifaa tiba Elizabeth Mollel akitolea ufafanuzi kwa wataalamu wa afya kuhusu namna ya kuripoti kupitia fomu na namba ya simu ya bure pindi inapotokea madhara wakati wa utumiaji wa vifaa tiba.
Na Fredy Mgunda, Iringa.
Mamlaka ya dawa na vifaa tiba [TMDA] Imetoa elimu ya kuhamasisha watumiaji wa vifaa tiba mkoa wa iringa ili kudhibiti madhara yatokanayo na vifaa tiba kupitia fomu na namba itakayotumika kutoa taarifa endapo kuna madhara yatajitokeza
Akizungumza wakati wa kutoa elimu hiyo afisa usajili wa dawa na vifaa tiba Bw. Felix Nzelote amesema kuwa wanatoa elimu hiyo ili kudhibiti athari zinazojitokeza kutokana na vifaa tiba huku akibainisha mahali mgonjwa atakapotoa taarifa ndapo atapata madhara
“Lengo ni kufikia wananchi au watumiaji wa vifaa tiba hapa nchini njia kubwa ni uhamasishaji katika vituo vyot vya kutola huduma na njia za kutoa taarifa kuna fomu zimeandaliwa ambayo ni ya orange ambayo tunakusanyia taarifa na namba ya free ambayo mtu atatumia ni 0800 110 084 pia USSD CODE ambayo ni *152*00# ambayo utaselect pale itakuja afya unachagua TMDA utaingia utaweka taarifa ya kifaa kilicholeta changamoto mgonjwa anapopata madhara no la kutoa huduma anatoa taarifa alafu muhudumu anamsaidia kujaza" alisema
Nzelote Godfrey mbangali ni mganga mkuu manispaa ya iringa na james joseph ni mratibu wa zoezi la utoaji wa elimu kimkoa walisema kuwa elimu hiyo itasaidia kutoa huduma iliyobora huku sababu ya athari za vifaa tiba visivyobora ikiwa ni sababu ya kuanzisha kufikisha limu hiyo
“Hii inatusaidia tuweze kutoa huma bora na wito kwa watoa huduma wote tuto taarifa kweny vituo vya iringa wakitoa hizi taarifa inatusaidia sisi kuwapa taarifa tmda na kuwza kudhibiti hivi vifaa tiba ili hivi vifaa viwe bora na tutatoa huduma bora vitndanishi vikiwa havina ubora tunawza kupata majibu ambayo sio sahihi mwanzo hakukuwa na sehemu maalumu ya kuripotia vil vitu vipo au huwa vinakuwepo lakini kwa kukosa sehemu ambayo tunaweza kutoa taarifa ndiyo ilisababisha watu wakaingia katika mgogoro wa namna ile wa wauguzi kukwazana na hii itatusaidia watoa huduma za afya itasaidia sana kwa wateja hata wanapowkewa vitu kwenda navyo nyumbani wanatambua ubora wake"alisema Mbangali
Kwa upande wake Mohammed Mang’una mganga mkuu Hospitali ya rufaa ya mkoa wa iringa alisema kuwa elimu hiyo iwe msaada wa kutambua muda wa matumizi ya vifaa tiba huku akiwataka wananchi kuchukua tahadhari pale vitakapopatikana vifaa tiba vilivyokwisha muda wake.
“Vile vifaa tiba huwa vinakuwa na muda wa kutumia na muda huo ukishafikia basi vinatakiwa kutafutiwa njia ya kuhifadhiwa ili visitumike tena sasamadhara yake kama tutakuwa tunandelea kuvitumia au hatujaviwka utaratibu mzuri basi vinaweza kuleta madhara kwa maana kuwa hatarishi kwa watumiaji either wagonjwa au hata wale wanao tumia kwa ajili ya wagonjwa wito wetu kwanza tuwe tayari kuupoka huu ujumbe pia tuwez kutoa ushirikiano pal ambapo tutakuwa tumepata vifaa tiba mbalimbali ambavyo tayari muda wake umkwisha wa kutumia na tukisma hivi sio vya kutumia wananchi wasije wakaona sehemu yoyote wasiviguse vitatupatia madhara"Alisema mang’una
Zoezi hilo linafanyika katika wilaya mbili za mkoa wa iringa manispaa ya iringa na mji wa mafinga huku TMDA ikitembelea vituo 12 vya vya afya vya serikali na binafsi
Post a Comment