Header Ads

test

TSN na Vijana Connect waungana kuwapa fursa za Maendeleo vijana

Na Karama Kenyunko Michuzi TV


KAMPUNI ya Magazeti ya Serikali (TSN) na Taaisi ya ‘Vijana Connect wamesaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kudumu wenye lengo la kuwajengea vijana uwezo wa kuibua fursa mbalimbali na kuweza kunufaika na fursa hizo katika kuendeleza shughuli za maendeleo ya jamii.

Akizungumza wakati wa hafla ya kutiliana saini kwa makubaliano hayo, iliyofanyika leo Machi 16, 2023 katika ofisi za TSN jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TSN, Lamau Mpolo amesema lengo la makubaliano hayo ni kuwajengea vijana uzalendo katika kutumikia fursa mbalimbali ikiwemo za uongozi, kilimo, mazingira na nyinginezo.

Amesema vijana wana wajibu wa kupanga maendeleo ya taifa, hivyo makubaliano hayo yatahakikisha yanachachua na kuanzisha mijadala itakayoleta Maendeleo kwa nchi ili kuhakikisha vijana wote nchini wanahusika na kuwajibika na shughuli zozote za maendeleo nchini

"Kupitia Jukwaa hili na wadau wengine ambao tutawashirikisha, tutahakikisha vijana wanashiriki kikamilifu katika kupanga Maendeleo ya nchi yao kwani vijana ambap ni nguvu kubwa wanawajibu wa kushiriki na kushirikishwa katika kupanga Maendeleo ya nchi. Amesema Mpolo

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Vijana Connect, Hamza Jabir amesema lengo la taasisi yao ni kuangalia fursa za kiserikali na siziso za kiserikali kwa lengo moja la kuwapa hamasa na kuwafaidisha vijana kupitia taasisi yao.

Amesema kuna vijana wengi wa maeneo mbalimbali ambao wamekuwa hawafikiwi na upatikanaji wa fursa hasa katika maeneo ya mikoani, lakini sasa kupitia makubaliano hayo wataweza vijana wengi wataweza kufikiwa na fursa za kupata taarifa na kuifanyia kazi.

“Tumekuwa na program mbalimbali kwa vijana nchi nzima, lengo ni kuwafikia vijana na namna gani wanaweza kutumia fursa, wapo vijana wengi ambao tumewafikia na tunaendelea kufanya hivyo”. Amesema Jabiri
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) Lamau Mpolo kulia na Mwenyekiti wa Vijana Connect,  Hamza Jabir wa pili kushoto wakionyesha hati ya hati ya mkataba wa makubaliano na ushirikiano wa kudumu wenye lengo la kusaidia na kuwajengea uwezo vijana ili kuweza kuibua fursa na kunufaika nazo katika shughuli  za Maendeleo ya Jamii. Wanaoshuhudia kushoto na kulia ni wafanyakazi kutoka TSN na Vijana Connect
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) Lamau Mpolo kulia na Mwenyekiti wa Vijana Connect,  Hamza Jabir wa pili kushoto wakisaini hati ya mkataba wa makubaliano na ushirikiano wa kudumu wenye lengo la kusaidia na kuwajengea uwezo vijana ili kuweza kuibua fursa na kunufaika nazo katika shughuli  za Maendeleo ya Jamii. Wanaoshuhudia kushoto na kulia ni wafanyakazi kutoka TSN na Vijana Connect

No comments