MTANDAO WA POLISI WANAWAKE TANZANIA (TPF-NET) WAMESHIRIKIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE JIJINI DODOMA
Na. Benedict Mlawa wa Jeshi la Polisi
Jeshi la Polisi kupitia Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF-NET) limeshiriki katika kuadhimisha
sherehe ya siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Machi 08, 2023 Wilayani Kondoa Jijini Dodoma.
Maadimisho hayo yameongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule leo Machi
08, 2023 ambaye ameongoza viogozi wa Kiserikali, Chama, Vyombo vya Ulinzi na Usalam, Taasisi ,
Mashirika, Dini Pamoja na Wananchi katika kuadhimisha ya siku ya Wanawake Duniani ambayo
imefanyika kimkoa Wilaya ya Kondoa Jijini Dodoma, ambapo maadhimisho haya yamebebwa na kauli
mbiu isemayo “Ubunifu na Mabadiliko ya Technolojia, chachu katika kuleta Usawa wa Kijinsia”
Mkuu wa Mkoa aliwashukuru na kuwapongeza viongozi na wakazi wa Wilaya ya Kondoa kwa maandalizi
mazuri waliyoyafanya kwa kuupokea ugeni mzima wa mkoa wa Dodoma katika wilaya yao.
Pia, Senyamule alisema anamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Daktari
Samia Suluhu Hassan kwa kuwa chachu ya mafanikio kwa Wanawake hapa nchini kwa kuamini kwamba
Wanawake wanaweza hata ukiangalia katika uteuzi wake waviongozi wanawake wamepewa nafasi
kwa kuamini usawa wa Kijinsia.
Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa Rosemary Senyamule aliwa taka wanawake kujitokeza na kuzifanyia kazi
fulsa mbalimbali ambazo zinatolewa serikali ili kuweza kufikia malengo ya Usawa wa Kijinsia kwa
maendeleo endelevu.
Pia, Mkuu wa Mkoa Rosemary Senyamule aliongeza kwa kusema Jamii lazima izingatie haki za watoto
wa kike kwa kumlinda mtoto wa kike dhidi ya ndoa za utotoni ili aweze kufikia na kufaidi huduma za
jamii ikiwa ni pamoja na kupata elimu yenye kuwezesha kudai na kumlinda mtoto wa kike dhidi ya
Ukatili wa Kijia.
Post a Comment