TAASISI ZATAKIWA KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA UTEKELEZAJI SHERIA YA MAZINGIRA
Taasisi zatakiwa kushughulikia changamoto za utekelezaji Sheria ya Mazingira
Ofisi ya Makamu wa Rais imetoa wito kwa taasisi zinazowajibika na utekelezaji
wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (EMA) ya mwaka 2004 zimetakiwa
kushughulikia changamoto za utekelezaji wake.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt.
Andrew Komba wakati akifungua Warsha ya Kupitia Taarifa ya Tathmini ya
Utekelezaji na Changamoto za Mfumo wa Kitaasisi na Kisheria wa EMA nchini.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Komba
amesema Serikali ya Tanzania ilichukua hatua ya kulinda na kuhifadhi mazingira
kwa kuweka Sera ya Taifa ya Mazingira (1997) na Sheria ya Usimamizi wa
Mazingira (EMA) (2004).
Amesema Sheria hiyo imeweka mfumo wa kiutawala na kitaasisi wa usimamizi
wa mazingira unaojumuisha ngazi zote za kiutawala katika Serikali unaojumuisha
Wizara na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
“Ndugu zangu washiriki wa warsha hii licha ya juhudi za Serikali za kusimamia
uhifadhi na wa mazingira, bado kuna changamoto na upungufu katika taasisi
zinazowajibika utekelezaji wa Sheria ya Mazingirakamili wa EMA.
“Hivyo, katika warsha hii mtapitia rasimu ya taarifa ya tathmini ya utekelezaji na
changamoto za mfumo wa kitaasisi na kisheria uliopo wa usimamizi wa mazingira
nchini,” amesema Dkt. Komba.
Ameongeza kuwa maoni kuhusu tathmini juu ya utekelezaji na changamoto za
mfumo uliopo wa kitaasisi na kisheria wa usimamizi wa mazingira utatoa
matokeo muhimu ya kuimarisha utekelezaji wa EMA kupitia upungufu
uliobainishwa.
Aidha, Mkurugenzi huyo amelipongeza na kulishukuru Shirika la Maendeleo la
Sweden (SIDA) kwa juhudi zake katika kushirika kuimarisha uwezo wa Taifa wa
utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira kupitia Mradi wa Kuimarisha
Uwezo wa Kitaasisi wa Utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (EMA).
Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Andrew Komba akifungua Warsha ya Kupitia Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji na Changamoto za Mfumo wa Kitaasisi na Kisheria wa EMA nchini kwa niaba ya Katibu Mkuu iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.
Post a Comment