Waliopata Division One St Anne Marie waula
Na Humphrey shao Michuzi Tv
WANAFUNZI zaidi ya 400 wa shule za St Anne Marie Academy, Brilliant na Sunshine ya Kibaha wamepewa zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslim na uongozi wa shule hiyo.
Wanafunzi hao walipewa zawadi hizo kwenye Bonanza lililoandaliwa mwishoni mwa wiki kwenye shule ya St Anne Marie Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam.
Miongoni mwa wanafunzi hao 400, wanafunzi 80 walipata Division 1.7 na wengine Division 1.8 hali ambayo iliifanya uongozi uone mumhimu wa kuandaa Bonanza hilo.
Akizungumza kwenye Bonanza hilo, Mkurugenzi wa shule hizo, Dk. Jasson Rweikiza alisema waliamua kuandaa Bonanza hilo kama motisha kwa wanafunzi zaidi ya 400 wa shule hizo waliopata daraja la kwanza kwenye mitihani ya kidato cha pili mwaka 2021 na 2022.
“Hili ni Bonanza la kusherehekea mafanikio tuliyoyapata mwaka jana na mwaka juzi mfululizo wanafunzi wetu wa kidato cha pili walifanya vizuri sana na tukaona haitakuwa vyema wala haki tukae kimya,”
“Tumeona tutambue ufaulu huu mzuri kama motisha kwa wanafunzi wetu. Kufundisha na kufaulisha kwa kiwango hiki siyo kazi rahisi ni kama vita na ukishinda vita silazima ufanye sherehe,” alisema Dk. Rweikiza
Alisema wanafunzi wa shule hizo tatu za St Anne Marie Academy, Sunshine na Brilliant walipata daraja la kwanza na wengine walipata daraja la kwanza la juu la 1.7 na 1.8.
“Leo jioni tumeandaa dansi hapa shuleni wanafunzi wa shule hizi tatu watacheza muziki kula na kunywa ili iwe motisha kwa wengine kusoma kwa bidii,” alisema Dk. Rweikiza
Mkurugenzi wa shule ya St Anne Marie Academy, Dk. Jasson Rweikiza, akimpa zawadi mwanafunzi wa shule hiyo, Ernest Junda aliyepata division 1.7 kwenye matokeo ya kidato cha pili mwaka jana. Halfa hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo kuwazawadia wanafunzi zaidi ya 400 wa shule za St Anne Marie, Brillliant na Sunshine waliopata daraja la kwanza kwenye mitihani ya mwaka 20221 na 2022.
W anafunzi wa shule ya sekondari Sunshine ya Kibaha, Abdulaziz Mwangi, (Kushoto) , Jesse Machemba (katikati) wa St Anne Marie Academy na Claud Mhagama wa sekondari ya Brilliant wakishindana kula chapati wakati wa Bonanza la Rweikiza mwishoni mwa wiki kwaajili ya kuwapa zawadi wanafunzi waliopata daraja la kwanza kwenye mitihani ya kidato cha pili mwaka 2021 na 2022.
Post a Comment