Header Ads

test

WAZIRI KIRUSWA ATEMBELEA MITAMBO YA KUZALISHA MKAA MBADALA

Na.Khadija Seif, Michuziblog

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wamefanya ziara ya kutembelea Kiwanda cha kutengeneza Makaa ya Mawe Kilichopo Shirika la Utafiti na teknolojia (TIRDO) Kwa kutazama namna hatua za awali za kutengeneza Makaa hayo pamoja na Mashine mbalimbali zinazotumika kufanya Uzalishaji.

Akizungumza na Wanahabari Leo Machi 20,20223 Wakati wakutembelea Mradi wa Kuzalisha Mkaa mbadala wa "Rafiki briquette" Naibu Waziri Steven Kiruswa amesema Mradi huo tayari umeshaonesha mafanikio makubwa na kuifanya Wizara ya Madini kuagiza Mashine kubwa ili kuendelea kufanya uzalishaji kwa kuweka baadhi ya Mikoa.

"Kibaha na Songwe tayari mitambo hiyo imewafikia na na kilichobaki baada ya hatua hiyo wakasimike na kuanza kufanya uzalishaji wa Tani 2000 kwa saa"amesema Kiruswa.

Aidha,amesema Mitambo mengine miwili inatarajiwa kufika na itapelekwa Kanda ya Kati Dodoma pamoja na Geita kutokana na maeneo hayo kuwa na ukataji wa Miti mingi kwa matumizi ya majumbani hivyo kuwepo kwa Mkaa huo mbadala itasaidia zaidi mahitaji ya Nishati bila ya kuwepo athari ya ukataji Miti.

"Tukianzisha Viwanda huko hata wale watu ambao walikua wanapata kipato huko watahamia kwenye uzalishaji wa mkaa mbadala na kuendelea na shughuli zao kwa vipato vyao vya uhakika".

Hata hivyo ameongeza kuwa ipo changamoto kutokana na kuchelewa kwa mitambo hiyo kufika nchini Tanzania sababu kubwa ikielezwa kuwepo kwa Ugonjwa wa UVIKO 19.

"Wakati tunafanya mpango wa kuagiza mitambo ndio kipindi ambapo Dunia ilikubwa na ugonjwa wa UVIKO 19 hivyo ikapelekea tusitishe kwa muda mpaka pale hali itakapotengemaa."

Ametoa wito kwa Serikali kutenga bajeti ili Uzalishaji uwe kwa wingi kwani kutumia Mkaa huo mbada una faida nyingi ikiwemo kuwanusuru watumiaji na madhara ya kifua pamoja na macho huku gharama za mkaa huu kuwa wa bei nafuu kwa watumiaji.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya ya STAMICO Meja Jenerali Mst.Michael Joseph Isamuyo amesema Mradi huo ni wa muda mrefu huku akieleza sababu ya mitambo hiyo na shughuli ya uzalishaji wa Mkaa mbadala kuzalishwa katika eneo la Shirika la Utafiti (TIRDO) ni sehemu ya Utafiti na teknolojia na itasaidiauzalishaji huo kuwa wa ufanisi zaidi.

"Mitambo iliyofika ilikua ni kwa ajili ya vitendo na kujiridhisha kuwa tunaweza kutengeneza mkaa mbadala bila kuleta athari na tulifanya Utafiti na kubaini kuna gesi na tuliongeza mashine kwa ajili ya uondoaji wa gesi hizo zisilete madhara kwa binadamu."

Pia amewatoa hofu watumiaji kuwa Mkaa huo mbadala umethibitishwa na Shirika la Viwango nchini kuwa ni mkaa bora na salama kwa matumizi.
Naibu Waziri wa Nishati,Steven Kiruswa akizungumza na Wanahabari mara baada ya kutembelea mradi wa Kuzalisha mkaa mbadala wa "Rafiki briquette " uliopo (TIRDO) Msasani Jijini Dar es salaam. 

No comments