WAZIRI ULEGA AAHIDI KUGAWA MITUNGI YA GESI KWA WALIMU SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI WILAYANI MKURANGA
Na Mwandishi Wetu Michuzi TV - Mkuranga
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mkoa wa Pwani Abdallah Ulega amesema atawapatia mitungi ya gesi walimu wa shule za sekondari na msingi wilayani ili nao wawe wanapika katika mazingira mazuri sambamba na kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu za kuhamasisha nishati safi ya kupikia.
Akizungumza wakati wa Kongamano la Wanawake Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani inayosherehekewa kila Machi 8 ya kila mwaka, Waziri Ulega amewahakikishia kuwapatia mitungi hiyo.
Katika maadhimisho hayo yaliyofanyika Mkuranga mjini, mgeni rasmi alikuwa ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya wa Wanawake wa CCM( UWT), Zainab Hamis Shomary na Ulega alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikuwa pia wa tukio hilo.
"Niwaahidi walimu wa Shule za Msingi na sekondari katika Wilaya yetu ya Mkuranga tutaapatia mitungi ya gesi ambayo ni nishati safi ya kupikia,hii itawafanya muwe mnapika katika majiko salama lakini wakati huo huo tutakuwa tunaunga mkono juhudi za Serikali inayoongozwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kutunza mazingira yetu,"amesema Ulega
Mbali na hilo, Ulega amewaahidi kuwawezesha wanawake waliohudhuria kongamano hilo na wasiokuwa kadi ya Bima ya Afya ya Jamii ili kuhakikisha wanapata matibabu kwa uhakika.Pia alisema suala hilo litawahusu wanawake wajumbe wa mkutano mkuu wa Mkuranga.
Katika kongamano hilo, Ulega alieleza kazi na shughuli zilizotekelezwa ndani ya miaka miwili chini ya uongozi wa Rais Samia, akitolea mfano katika sekta ya elimu, afya, miundombinu ya barabara.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mkoa wa Pwani,Abdallah Ulega akizungumza wakati wa Kongamano la Wanawake Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani inayosherehekewa kila Machi 8 ya kila mwaka.(PICHA NA EMMANUEL MASSSAKA WA MICHUZI TV)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mkoa wa Pwani ,Abdallah Ulega akimkabidhi zawadi Makamu Mwenyekiti wa umoja wa Wanawake Tanzania, Zainabu Shomari
Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mkoa wa Pwani ,Abdallah Ulega akipokea zawadi wakati wa Kongamano la Wanawake Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani inayosherehekewa kila Machi 8 ya kila mwaka.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Mkoa wa Pwani,Mariam Ulega (kulia) akimpa zawadi Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania, Zainabu Shomari (kushoto)
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Mkoa wa Pwani,Mariam Ulega akiwa katika piha ya pamoja na wadau jukwaa hilo.
Matukio mbalimbali
Makamu wa Umoja wa Wanawake Tanzania, Zainabu Shomari (kushoto) kutoka ukumbini huku akisindikizwa na wanawake wa Mkoa wa Pwani.(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA WA MICHUZI TV)
Post a Comment