WAKUU WA MIKOA DHIBITINI MAAMBUKIZI YA MALARIA-MAJALIWA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa mikoa ambayo ina kiwango kikubwa cha Maambukizi ya Malaria ianze kusimamia utekelezaji wa afua za ugonjwa huo ili kupunguza viwango hivyo.
Amesema kuwa lengo la Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kutokomeza maambuzi ya ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030 “Upatikanaji wa afua za kinga kama vyandarua vyenye dawa na upatikanaji wa vitendanishi na dawa za malaria utasaidia sana kupungua kwa idadi ya wagonjwa na vifo vitokanavyo na Malaria hapa nchini”
Ametoa wito huo leo Jumanne (Aprili 25, 2023) wakati alipomuwakilisha Rais Dkt. Samia Sukuhu Hassan katika Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani kwa Mwaka 2023 ambapo Kitaifa yamefanyika Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu amesema takwimu zinaonesha mikoa inayoongoza kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya Malaria ni Tabora una asilimia 23, Mtwara asilimia 20, Kagera asilimia 18, Shinyanga asilimia 16 na Mkoa wa Mara una asilimia 15.
“Kwa upande mwingine, nimeelezwa kuwa mikoa 9 ina kiwango cha maambukizi chini ya asilimia moja nayo ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Singida, Dodoma, Songwe, Iringa, Dar es salaam na Mwanza. Kwa namna ya pekee kabisa ninaipongeza sana mikoa yote iliyofanikiwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya Malaria”
Ameongeza kuwa takwimu zilizopo zinaonesha kuendelea kupungua kwa maambukizi ya Malaria mwaka hadi mwaka kutoka asilimia 14.8 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 8.1 mwaka 2022. “nitoe wito kwa kuendelea kuongeza nguvu katika mapambano ya kutokomeza Malaria”
Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ameitaka Wizara ya Afya kufanya kampeni ya kutosha katika kuhamasisha matumizi ya vyandarua vya kisasa hadi maendeo ya vijijini “hakikisheni afua hii inaanza kutekelezwa katika Mikoa yenye kiwango cha maambukizi chini ya asilimia moja ili tuweze kuharakisha ufikiwaji wa malengo ya kutokomeza ugonjwa wa Malaria hapa nchini”
“Naipongeza Wizara ya Afya kwa dhamira ya dhati katika mapambano dhidi ya malaria nchini Tanzania. Hivi sasa, zaidi ya 98% ya kesi za malaria zinathibitiwa, kesi za malaria zilizothibitiwa kwa mwaka zinaonesha kati ya kila watu 1,000 zilipungua kutoka 106 mwaka 2020 hadi 76 mwaka 2021 na zaidi hadi 58 mwaka 2022”
Nape Nnauye Vyombo vya habari, Mitandao ya kijamii hakikisheni mnakuwa na mpango endelevu wa kuifanya Tanzania inakuwa na 0 ‘Zero’ Malaria kila mmoja ahakikishe anatimiza wajibu wake.
Naye, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kuwa Wizara hiyo kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria na kwa kushirikiana na Wadau pamoja na Ofisi ya Rais - TAMISEMI inatekeleza Mpango Mkakati wa Malaria wa kipindi cha miaka mitano (5) kuanzia mwaka 2021 hadi 2025.
Amesema kuwa mpango Makati huo unalenga kupunguza kiwango cha maambukizi ya malaria nchini kutoka wastani wa asilimia 7.5 ya mwaka 2017 hadi kufikia wastani wa chini ya asilimia 3.5 ifikapo mwaka 2025.
“Mkakati wa udhibiti wa mbu waenezao malaria unatekelezwa kupitia afua kuu nne za ugawaji na matumizi ya vyandarua vyenye dawa, upuliziaji viuatilifu ukoko kwenye kuta ndani ya nyumba, utunzaji na udhibiti wa mazingira ili kuondoa mazalia ya mbu pamoja na unyunyiziaji wa viuadudu vya Kibaiolojia kwenye mazalia ili kua viluwiluwi vya mbu”
Naye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ametoa wito kwa Vyombo vya habari, Mitandao ya kijamii na makampuni ya simu kuhakikisha wanakuwa na mipango endelevu ya kuifanya Tanzania inakuwa na Ziro’ Malaria “kila mmoja ahakikishe anatimiza wajibu wake”
Akizungumza Kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Angellah Kairuki, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dkt Wilson Mahela amesema kuwa Ili kufanikisha mapambano dhidi ya Malaria, TAMISEMI imeendelea kusimamia utekelezaji wa Afua kinga na Afua tiba zinazotekelezwa Nchini.
Amesema kuwa katika kutekeleza Afua kinga, OR-TAMISEMI inasimamia mazoezi ya ugawaji wa vyandarua katika vituo vya kutolea huduma,mashuleni,kwa makundi maalumu(wazee wenye umri kuanzia miaka 60 na zaidi,watoto wenye umri chini ya miaka 5 waliolazwa na Malaria kali”
Naye, Muwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani nchini Dkt. Zabulon Yoti ameipongeza Tanzania kwa kuwa moja kati ya mataifa manne Afrika katika kupunguza vifo duniani vitikanavyo na malaria kwa asilimia 52 ikiungana na nchi za Nigeria, Niger na Congo huku Tanzania ikirekodi asilimia Nne tu ya vifo.
Post a Comment