Header Ads

test

RC MAKALLA: KAMPENI YA SAFISHA PENDEZESHA DSM IMESAIDIA KUTOKOMEZA MALARIA.

 




Mkoa wa Dar es salaam ni Moja ya mikoa 7 inayofanya vizuri katika Mapamanno ya malaria.

Awakumbusha wananchi kusafisha mitaro, kufyeka majani , kufukua madimbwi, mazalia ya mbu Na kutumia vyandarua kutokomeza malaria.

Amshukuru Rais Dkt, Samia kwa kutoa zaidi ya Shilingi bilioni 30 kwaajili ya maboresho sekta ya Afya DSM.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam CPA. Amos Makalla amesema Mkoa huo umeendelea kufanya vizuri katika Mapamanno dhidi ya Malaria kutokana na kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM iliyosaidia kuweka Jiji katika Hali ya usafi.

RC Makalla amesema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani ambapo kitaifa yamefanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo Mgeni rasmi ni Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.

Aidha RC Makalla amesema kupitia kampeni hiyo mazingira yamekuwa safi baada ya kuamgamiza mazalia ya mbu kufuatia usafi wa Mitaro, ufekaji Vichaka, na kufunika Madimbwi ya Maji.

Kutokana na Mafanikio hayo, RC Makalla ametoa wito kwa Wananchi kuendelea kufanya usafi wa mazingira wanayoishi ikiwa ni pamoja na kulala kwenye vyandarua Ili kutokomeza malaria.

Pamoja na hayo RC Makalla amemuhakikishia Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kuwa Mkoa huo utaendelea kufanya vizuri katika Mapamanno dhidi ya malaria kwa kutoa elimu ya kutosha ya kujikinga.

Hata hivyo RC Makalla amemshukuru Rais. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zaidi ya Shilingi bilioni 30 kwaajili ya maboresho ya huduma za Afya kwenye Mkoa huo ikiwemo ujenzi wa Hospital, Vituo vya Afya na Zahanati.

No comments