Header Ads

test

BancABC Tanzania kuendelea kuwekeza kwenye bidhaa na huduma bunifu.

Dar es Salaam Jumanne 11 Aprili 2023… Benki ya BancABC Tanzania, ambayo ni Kampuni
tanzu ya Atlas Mara imesema itaendelea kuwekeza kwenye bidhaa na huduma bunifu ili
kuendana na hali halisi ya maisha ya kila ya wateja wake. Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Tanzania Imani John wakati wa
futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake.

BancABC Tanzania iliandaa futari hiyo ambayo ilileta watu Zaidi ya 300 na kuongozwa na
Kaimu Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Walid Al-hadi Omar ambaye alitoa wito
kwa Watanzania wote bila ya kujali dini zao kuonyesha Umoja na mshikamano wakati huu wa
mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

‘Tumeandaa futari hii ili kuonyesha Umoja na vile tunavyowajali wateja wetu’, alisema Iman
huku akisema kuwa benki hiyo imekuwa na utamanduni wa muda mrefu wa kuandaa futari ikiwa
ni ishara ya kuonyesha upendo kwa kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

‘Tumekuwa na utamanduni wa kuandaa futari kila mwaka kama ishara ya kuonyesha upendo
kwa wateja wetu kama ishara ya kuonyesha upendo na uaminifu wao kwa kuchangua sisi kama
benki yao’, alisema Imani huku akiongeza kuwa matukio kama haya ya futari ni muhimu kwani
pia ni muda muafaka wa kuongea na wateja na kujua mahitaji yao’.

Akizungumzia kuhusu bidhaa na huduma ambazo utolewa na benki hiyo, Imani alisema ‘Sisi
BancABC tumekuwa tukitoa huduma na bidhaa ambazo zinanguza Watanzania wa kanda zote
kama vile wateja binafsi, wajasiriamali wadogo na wakubwa pamoja na wateja wakubwa
ambazo ni huduma za kuweka na kutoa fedha pamoja na mikopo nafuu.

‘Huduma na bidhaa zetu hizi ni za ubunifu wa hali ya juu na kutaendelea kuwekeza kwenye
ubunifu ili kuendana na hali halisi ya maisha ya kila Mtanzania’, alisema Imani.

Imani aliongeza kuwa BancABC imejikita kwenye huduma za kimtandao “kidijitali” ili
kuwezesha Watanzania wengi walio nje na ndani ya nchi kuendelea kufanya miamala na kukuza
pato la Taifa. Alitaja baadhi ya huduma hizo ni Pamoja na kadi za malipo ya awali “pre-paid

card” kwa sarafu tano tofauti ikiwemo TZS, USD, GBP, EUR na Yuan ya Uchina, huduma za
kibenki kwa njia ya simu za mkononi yani “Mobile Banking”.

Huduma zingine ni huduma za kibenki kwa njia ya Internet yani Internet Banking ambapo mteja
anaweza kufanya muamala na kutizama salio lake akiwa nyumbani au ofisini kwake kwa
usalama kabisa, Malipo ya Serikali kwa njia za kimtandao yaani GEPG pamoja na huduma za
kifedha kwa njia za Mawakala maarufu kama Agency Banking

Kwa upande wake, Kaimu Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Walid Al-hadi Omar
aliipongeza BancABC Tanzania kwa kuandaa futari huku akisema ni ishara ya kuonyesha
upendo kwa jamii ya Waislamu. ‘Kuandaa futari hii sio tu kuonyesha upendo kwa wateja wenu
lakini pia ni ishara ya upendo kwa jamii ya waislamu wote na vizuri kwani waislamu kwenye
mwezi Mtukufu kuandaliwa futari ni ishara ya upendo na kuthaminiwa’, alisema Sheikh Omar
huku akitoa wito kwa Watanzania wote bila kujali dini zao kuendelea kuonyesha Umoja na
mshikamano na hasa kwa kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

‘Naomba nichukue fursa hii kuwashukuru BancABC Tanzania kwa kuweza kuunga mkono jamii
yetu na sana sana kwa jamii yenye ulemavu kwani ni mfano kuwa benki hii imejikita kwenye
kuguza maisha ya kila Mtanzania.

‘Ni kawaida kwa mashirika ya kifedha kuwekeza sehemu ambayo wana uhakika wa kurundisha
faida. Lakini BancABC imeonyesha utofauti kwani imeenda hatua mbele na kwa kweli huu ni
mfano wa kupongezwa’, alisema Omar huku pia akiipongeza benki hiyo kwa kuendelea kuunga
mkono miradi ya maendeleo na hasa kwa Mkoa wa Dar es Salaam.



Kaimu Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Walid Al-hadi Omar (kulia) na
Mkurungezi Mtendaji wa BancABC Tanzania Imani John wakiwaongoza wateja na wafanyakazi
wa benki ya BancABC Tanzania kwenye futari iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo na shukrani hasa kwa wale ambaowako kwenye mfungo kwa kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Tanzania Imani John (kulia) akimkabidhi zawadi kwa
Kaimu Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Walid Al-hadi Omar wakati wa futari
iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurungezi Mtendaji wa BancABC Tanzania Imani John (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM
Mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtevu (kulia) wakiwaongoza wateja na wafanyakazi wa benki
ya BancABC Tanzania kwenye futari iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni
mwa wiki ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo na shukrani hasa kwa wale ambao wako kwenye
mfungo kwa kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Kaimu Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Walid Al-hadi Omar akiwaongoza
wateja na wafanyakazi wa BancABC Tanzania kwenye futari iliyoandaliwa na benki hiyo jijini
Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo na shukrani hasa kwa
wale ambao wako kwenye mfungo kwa kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Tanzania Imani John (kulia) akimkabidhi zawadi kwa
Kaimu Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Walid Al-hadi Omar wakati wa futari
iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


No comments