Hafla ya Utoaji Mikopo na Mifano ya Hundi Kwa Vikundi Mbalimbali
Naibu waziri wa elimu sayansi na teknolojia MH. OMARY KIPANGA ambnae pia ni mbunge wa jimbo la Mafia mkoani Pwani amevitaka vikundi mbalimbali, vya wajasiriamali vilivyonufaika na mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na halmashauri kuhakikisha wanaitunza mikopo ikiwemo kurejesha kwa wakati mikopo wanayopatiwa na halmashauri ili kutoa fursa kwa vikundi vingine kupatiwa mikopo hiyo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi hundi yenye thamani ya zaidi ya shilingi million Milioni Mia moja , tisini na tatu, laki tisa na elfu kumi na mbili, boda boda 23, mashine mbalimbali ikiwemo ya kuranda mbao, mashine ya kutengeneza maumbo mbalimbali na vifaa vingine vya ujasiriamali.

Nae mkuu wa wilaya ya Mafia ZEFANIA SUMAYE akiwaasa wanufaika wa mikopo hiyo kuitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ili iweze kuwanufaisha lakini pia kutoa fursa kwa wengine kukopa.
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya Mafia KASSIM NDUMBO amesema anajivunua mafanikio yaliyopatikana kupitia mikopo hiyo ikiwa ni pamoja wananchi wa Mafia kuinuka kiuchumi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya Mafia KASSIM NDUMBO amesema anajivunua mafanikio yaliyopatikana kupitia mikopo hiyo ikiwa ni pamoja wananchi wa Mafia kuinuka kiuchumi.
Mikopo hiyo ya asilimia kumi inayotelewa kupitia makusanyo ya ndani imetolewa kwa vikundi vya wajasiriamali vya wanawake , vijana na watu wenye ulemavu.
Matukio mbalimbali katika Picha Katika Hafla ya Utoaji Mikopo na Mifano ya Hundi Kwa Vikundi Hafla iliyoongozwa na Mbunge wa Jimbo la Mafia Mhe Omar Juma Kipanga QS Ambae pia ni Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Tanzania
Post a Comment