JUVE WATAWAZWA MABINGWA WA POLISI CUP
Na.Khadija Seif, Michuziblog
LIGI ya Polisi jamii kwa Mkoa wa kipolisi Kinondoni imemalizika baada ya timu ya Juve kutoka Msasani kuibuka Washindi kwa mabao mawili dhidi ya Kijitonyama combine bao moja.
Akizungumza mara baada ya mtanange huo kurindima Katibu Tawala Wilaya ya Kinondoni Stelah Msofe amesema lengo la mashindano hayo ni kuhakikisha Jamii hususani vijana wanapata Uwelewa mkubwa dhidi ya uhalifu na kujenga ushirikiano na jamii kwani ndiyo husaidia kupatikana taarifa za wahalifu
"Washindi wote katika kinyang'anyiro hiki watapata zawadi isipokuwa Mshindi wa Kwanza ataondoka na mbuzi wawili,Jezi,Kikombe na mpira hii ni kuwapa hamasa vijana wengine wanaposikia mashindano kama haya washiriki "amesema Msofe
Hata hivyo Msofe amesema kuwepo kwa michezo hiyo inaleta mahusiano mazuri kati ya raia na jeshi la polisi ili kuweza kueleza changamoto mbalimbali kwenye mitaa yao pasipo kuweka dhana ya kuwa jeshi la Polisi ni watu wakorofi.
Naye Mwakilishi Jeshi la Polisi Kinondoni Kamanda Mtatiro Kitinkwi amesema mashindano hayo yalianzishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchi nzima kupitia kaminsheni Ushirikishwaji wa Jamii kule Mkoani Dodoma na yaliasisiwa kufanyika nchi nzima .
"Kuna njia mbalimbali zinazotumika kupambana na Uhalifu hivyo tunajua kwamba bila Jamii sisi Jeshi la Polisi hutuwezi kupambana na Uhalisi hiki kinachofanyika hapa kupitia mashindano haya hata tutakapo hitaji taarifa za wahalifu tunazipata haraka"amesema.
Pia akatoa ahadi kuwa Ligi hiyo kwa msimu ujao itafanyika kwa ukubwa zaidi ili kuendelea kuhamasisha ushirikiano kati ya raia na jeshi la Polisi pamoja na kuimarisha michezo.
Hata hivyo Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji wilaya ya Ilala Mohamed Balhabou amesema kutokana na kasi ya Rais Dkt.Samia Suluhu kuhakikisha michezo kwa sasa inafanya vizuri ni wajibu hata viongozi wa ngazi ya chini kutumia mfumo huo huo ili kuwepo na misingi mizuri kwa vijana kimichezo.

" Hata viongozi wa ngazi za chini hatujalaza damu kwenye michezo tutahakikisha tunaendelea na mfumo wa Rais wetu ili kuhakikisha Vijana wanashiriki michezo mbalimbali na tunaendelea kuwaunga mkono kwenye michezo ."
Katibu Tawala Wilaya ya Kinondoni Stelah Msofe akikabidhi Zawadi ya Kombe kwa Mabingwa wa Ligi ya Polisi jamii Juve kutoka Msasani mara baada ya kuwapa kichapo cha bao mbili Kijitonyama combine
Picha ya Pamoja ya Katibu Tawala Wilaya ya Kinondoni Stelah Msofe, Kamanda wa Polisi kutoka Mkoa wa Kinondoni Mtatiro Kitinkwi, na Viongozi mbalimbali akiwemo Diwani wa Kata ya Msasani Lucas Neghest,Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji wilaya ya Ilala Mohamed Balhabou na polisi kutoka Mkoa wa Kinondoni.
Post a Comment