Header Ads

test

DAR ES SALAAM WAFANYABIASHARA WA MIFUGO WATAKIWA KUFUATA TARATIBU KUUZA MIFUGO

Na. Mwandishi wetu Jeshi la Polisi

Wafanyabiashara wa mifugo nchini wametakiwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa
za kununua na kuuza mifugo ili kuepusha changamoto ambazo zinaweza kujitokeza hususani za
kununua mifugo ya wizi.

Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo Nchini Kamishna
Msaidizi wa Polisi ACP Simon Pasua wakati alipotembelea mnada wa kimataifa wa Pugu
pamoja na Machinjio ya Vingunguti Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhakikisha mifugo yote
inayouzwa ni halali kuelekea sikukuu ya Pasaka.

ACP Pasua amewataka wafugaji na wafanyabiashara wa mifugo kuhakikisha wanapelekea
mifugo yao katika minada ya Serikali ili kudhibiti matukio ya wizi.

Sambamba na hilo pia ametoa onyo kwa wafanyabiashara wachache ambao wanakwepa
kupeleka mifugo maeneo ya minada kuacha mara moja kwani jeshi hilo litaendelea kuwakamata
na kuwachukulia hatua za kisheria.

Pia ametoa wito kwa wafanyabiashara kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi kama kutatokea tukio
la wizi wa mifugo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanyabishara wa Mifugo katika machinjio ya Vingunguti
Bwana Joel Meshack amesema kutokana na elimu na maelekezo waliyoyapata changamoto
mbalimbali zilizokuwa zinawakabili zinaenda kutatuliwa.

Naye Daktari Mkuu wa Mifugo katika Mnada wa Pugu Bwana Ayoub Mollel amesema mara
zote wamekua wakishirikiana na Jeshi la Polisi kwa kukamata na kuzui mifugo yote
inayobainika kuwa ni ya wizi katika mnada huo.









No comments