TANROADS KUPITIA WAKANDARASI WAZAWA, YAKAMILISHA UJENZI WA BARABARA KWA KIWANGO CHA LAMI RUDEWA-KILOSA (KM 24)
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami Dumila-Kilosa-Mikumi sehemu ya RUDEWA-KILOSA yenye urefu wa kilometa 24 umefikia asilimia 90 ambapo mradi huo unatarajiwa kukamilika Julai, mwaka huu.
Kazi iliyobakia ni ujenzi wa madaraja matatu huku ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami ikiwa imekamilika na kuendelea kutumika.
Hayo yamesemwa Aprili 16, 2023 na Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Morogoro Mhandisi Mussa Kaswahili akitembelea miradi ya Rudewa-Kilosa na daraja la Kiyegeya lililopo wilayani Gairo ambapo amesema barabara hiyo ni sehemu ya barabara ya mkoa huo ambayo inaanzia Dumila hadi Mikumi.
Mhandisi Kaswahili ameongeza kuwa, hapo awali watumiaji wa barabara hiyo walikuwa wanatumia muda mrefu barabarani hadi kufika wakitokea Dumila kwenda Rudewa au Kilosa kutokana na ubovu wa barabara iliyokuwepo.
"Hapo awali kabla ya
Post a Comment