Header Ads

test

BANK OF AFRICA-TANZANIA KUWEZESHA WAKANDARASI NCHINI KUFANIKISHA MIRADI YAO YA UJENZI KWA UFANISI

Bank of Africa- Tanzania imewahakikishia Wakandarasi nchini upatikanaji wa mikopo na Dhamana za Benki, ambazo zitawarahisishia vigezo vya kupata mikataba mbalimbali na hatimaye kufanikisha miradi yao kwa ufanisi mkubwa.

Meneja wa Kitengo cha utoaji fedha za Biashara wa Bank of Africa Tanzania, Jessica Mizambwa, ameyasema hayo wakati benki hiyo iliposhiriki Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Bodi ya Wasajili wa Makandarasi uliomalizika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

"Benki inatoa huduma maalum ambazo ni suluhisho katika kufadhili miradi mbalimbali ya wakandarasi, huduma hizo zinazotolewa na benki yetu ni pamoja na; Dhamana ya Zabuni inayotoa dhamana ya hadi TZS Bilioni 1 ndani ya saa 24, Dhamana ya Malipo ya Mapema, Dhamana ya Utendaji kazi, punguzo la ankara, mikopo na nyinginezo na zinapatikana kwa haraka” Amesema Mizambwa.

Amesema huduma za kifedha kusaidia biashara zinalenga kukuza ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi yetu kwa kuwezesha usafirishaji wa bidhaa kuvuka mipaka na hata ndani, hivyo, Benki inawezesha wafanyabiashara wa aina mbalimbali ikiwemo wakandarasi, waagizaji bidhaa kutoka nje, na wauzaji bidhaa nje ili kuweza kupunguza uwezekano wa kupata hasara zinazohusiana na kufanya biashara za nje ya nchi.

Jessica, ameongeza kuwa, kupitia mpango wa benki wa kuwezesha wakandarasi, hasa wadogo, wanaweza kupata mashine bora za kufanyia kazi na kuweza kufanikisha kutekeleza miradi yao “ Bank of Africa Tanzani itawawezesha wakandarasi kupata mashine na kuondoa tatizo la wakandarasi kushindwa kutoa huduma kwa kukosa mashine au fedha". Amesisitiza.

Mgeni Rasmi katika mkutano huo, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi, Godfrey Kasekenya, amewataka wakandarasi wazawa wote nchini kuwa mabalozi wazuri kwa kufanya kazi nzuri kwa kuzingatia viwango na kukamilisha miradi kwa wakati ili Serikali ipate thamani ya fedha katika miradi yote.

Kasekenya ameeleza kuwa Wakandarasi wana mchango mkubwa katika kuinua uchumi wa nchi yetu na inapotokea Wakandarasi wanashindwa kutimiza wajibu wao wanachelewesha wananchi kupata huduma zilizokusudiwa na pia kuisababishia hasara Serikali.

Meneja Mahusiano wa Bank of Africa Tanzania, Edward Sam akitoa maelezo ya huduma zinazotolewa na Benki kwa mmoja wa washiriki aliyetembelea banda la Benki hiyo wakati wa mkutano huo.
Wafanyakazi wa Bank of Africa- Tanzania wakiwa katika banda lao.
Meneja wa Kitengo cha utoaji fedha za Biashara wa Bank of Africa Tanzania, Jessica Mizambwa (kulia) akipokea tuzo kwa niaba ya Benki kutoka kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi. Godfrey Kasekenya kutokana na bnchenki hiyo kushiriki katika mkutano wa mwaka wa Bodi ya usajili wa wakandarasi uliomalizika jijini Dar es Salaam, wengine pichani ni maofisa kutoka Bodi hiyo.Meneja wa Kitengo cha utoaji fedha za Biashara wa Bank of Africa Tanzania, Jessica Mizambwa (kulia) akipokea tuzo kwa niaba ya Benki kutoka kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi. Godfrey Kasekenya kutokana na benki hiyo kushiriki katika mkutano wa mwaka wa Bodi ya usajili wa wakandarasi uliomalizika jijini Dar es Salaam, wengine pichani ni maofisa kutoka Bodi hiyo.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi. Godfrey Kasekenya,(katikati kulia) akipata maelezo ya huduma zinazotolewa na Bank of Africa Tanzania kutoka kwa Meneja wa Kitengo cha utoaji fedha za Biashara, Jesca Mizamba wakati alipotembelea banda la maonyesho la benki hiyo kwenye mkutano wa mwaka wa Bodi ya usajili wa wakandarasi uliomalizika jijini Dar es Salaam.

No comments