Header Ads

test

MKATABA WA AWAMU YA PILI DMDP WASAINIWA KWA AJILI YA UTEKEKEZAJI WA MIUNDOMBINU WA JIJI LA DAR ES SALAAM.

Na Janeth Raphael - MichuziTv - Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Angellah Kairuki ameshuhudia utiaji saini wa mikataba ya kusanifu Mradi Uendelezaji wa Mkoa wa Dar es Salaam (DMDP) unaotarajiwa kuanza kutekelezwa Aprili 2024 na utagharimu Sh.Bilioni 800.

Akizungumza leo jijini Dodoma mara baada ya kushuhudia utiaji saini huo, Waziri Kairuki amewataka Wakandarasi hao kuzingatia masharti ya mikataba yao na wasiwe kikwazo kwenye utekelezaji wa mradi huo.

Kairuki amewataka wataalamu walio Saini mikataba wa mradi wa uboreshaji miundombinu mkoa wa Dar - es- salam awamu ya pili DMDP Kuhakikisha wanafanya kazi kwa usanifu na kutambua kuwa nafasi hiyo wamepewa kutokana na vigezo walivyo navyo huku akisisitiza kuwa fedha hizo zinazotolewa kukamilisha miradi ya utengenezaji wa miundombinu hiyo ni mkopo hivyo lazima ulipwe kwa wakati.

'Nitahakikisha nafatilia mradi huu kwa makini na kama kutatokea changamoto zozote mrudi katika mkataba kuangalia masharti ya kiutendaji yaliyowekwa na ikibainika Kuna utofauti hatua za Kisheria zitachukuliwa" - Amesema Waziri Kairuki.

Aidha amesema kuwa changamoto nyingi zilizopo katika Mkoa wa Dar es-Salam ni miundombinu ya barabara pamoja na mabadiliko ya tabia Nchi hivyo kama Serikali ya awamu ya sita imejipanga kutatua tatizo hilo kwa wananchi wake.

Pia amezitaka halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam wahakikishe changamoto zilizojitokeza Katika ujenzi wa awamu ya kwanza zisijitokeze awamu ya pili.

Kwa upande wake waziri wa fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa kupitia ofisi yake atahakikisha anafuatilia ujenzi huo kwa ukaribu na kwa makini Ili ufanikiwe.

Awali Mratibu wa miradi ya Serikali kupitia mikopo ya Benki ya Dunia Tamisemi na Tarura Mhandisi Humphrey Kanyenye amesema kuwa changamoto kubwa inayoikumba Jiji la Dar es salaam ni pamoja na ukosefu wa miundombinu ya barabara Katika maeneo ya mitaa na ukosefu wa mitaro ya maji taka Katika Jiji hilo, pamoja na usimamizi wa Mpango miji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Angellah J. Kairuki akiwa na  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu L. Nchemba pamoja na viongozi wengine wakishuhudia utiaji saini wa mkataba wa mradi wa uendelezaji Jiji la Dar es Salaam awamu ya pili (DMDP 2) katika Manispaa za Temeke na Kigamboni chini ya Mhandisi Consultancy Ltd & Luptan katika hafla hiyo fupi iliyofanyika ukumbi wa Mkapa jijini Dodoma tarehe 30 Mei, 2023.

No comments