RC SINGIDA :UKAMILISHAJI WA MIRADI YA MAENDELEO NI JAMBO LA KUFA NA KUPONA
Mkuuwa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akizungumza na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida wakati alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mkhandi kilichopo wilayani humo leo May 30, 2023. Kulia ni Mkuu wa wilaya hiyo, Mhandisi Paskas Muragili na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Omari Mande.
........................................................
Na Dotto Mwaibale, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida,Peter Serukamba amesema
kazi ya kumalizia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika wilaya zote mkoani
hapa ni la kufa na kupona na kuwa kazi hiyo ifanyike usiku na mchana kutokana
na umuhimu wake.
Serukamba ameyasema hayo leo May 30, 2023 wakati
alipokuwa katika mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea na kukagua ukamilishaji
wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida na kuhimiza
miradi yote iwe imekamilika kabla ya Julai 1, 2023 kwa viwango vinavyotakiwa na
kulingana na thamani halisi ya fedha zilizotolewa.
" Mkurugenzi, Mkuu wa wilaya, Madiwani,
Mhandisi na timu yenu nzima msikae ofisini nendeni ilipo miradi na hakikisheni ukamilishaji
wake unakuwa ndani ya siku 20 kuanzia leo na si vinginevyo kwani fedha zote
zitakazo salia kabla ya kuikamilisha zitarudishwa serikalini mwisho wa mwaka wa
fedha wa 2022/ 2023 ambapo zimebaki siku 20 tu
kuanzia leo,” alisema Serukamba.
Serukamba alisema hatapenda kuona fedha hizo
zikirudi bila ya kumaliza kazi iliyokusudiwa ya kumaliza ujenzi wa miradi hiyo
yakiwemo madarasa, zahanati na mabweni kwani kurudi kwa fedha hizo Rais Dk. Samia
Suluhu Hassan aliyezitoa hatakuwa ajatendewa haki pamoja na wananchi ambao ndio
walengwa wa miradi hiyo.
Aidha, Serukamba alisisitiza vituo vya afya na
zahanati zinazoendelea kujengwa ujezi wake uwe umekamilika kabla ya Julai na
Julai Mosi, 2023 zizinduliwe rasmi na kuanza kutoa huduma za afya kwa wananchi.
Alisema agizo la kukamilisha miradi hiyo kabla ya
Julai, 1, 2023 kwa halmashauri zote nchini zimetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Angellah Kairuki na
ndio maana wapo katika ziara ya kuhimiza kukamilika kwa miradi hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Singida, Omari Mande akizungumza kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo alisema
maagizo yote aliyoyatoa Mkuu wa Mkoa watayatekeleza kama walivyoagizwa na kuwa
hakuna mradi hata mmoja ambao hautakamilika ndani ya muda huo.
Miradi aliyoitembelea leo ni ujenzi wa zahanati
ya Kijiji cha Makhandi ambayo ujenzi wake ulianza mwaka 2019 kwa nguvu za
wananchi kwa ushirikiano wa vijiji viwili vya Makhandi na Idd Simba, ujenzi wa
bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari ya Maghojoa ambapo Mkuu wa Mkoa
Serukamba aliomba halmashauri hiyo itumie fedha zake za ndani kwa ajili ya
kuingiza umeme na maji.
Mradi mwingine uliokaguliwa ni ujenzi wa Zahanati
ya Kijijicha Sagara, ujenzi wa bwalo la chakula katika Shule ya Sekondari ya
Itaja, Ujenzi wa vyoo katika Shule ya Msingi ya Mwighanji, ujenzi wa bweni la
wasichana katika Shule ya Sekondari ya Mughanga, ujenzi wa bweni kupitia mradi
wa elimu maalum.
katika
Kijiji cha Mgori, ujenzi wa darasa katika Shule ya Msingi Mughamo na ujenzi wa
nyumba ya walimu katika Shule ya Msingi Ngaramtoni.
Katika ziara hiyo Serukamba aliongoza na wakuu wa
idara, maafisa watendaji wa kata na Tarafa, wataalam na wajumbe wa kamati ya
ulinzi na usalama wa wilaya hiyo.
Kesho Mkuu wa Mkoa Peter Serukamba anatarajia kuendelea na ziara yake hiyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuhimiza ukamilishwaji wake kwa wakati.
Mkuu wa wilaya hiyo, Mhandisi Paskas Muragili, akisisitiza jambo wakati wa ukaguzi wa Zahanati ya kijijihicho.
Post a Comment