RPC TANGA AWATAKA WAENDESHA BODABODA KUTII SHERIA
Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Henry Mwaibambe akizungumza na wamiliki,waendesha bodaboda na bajaji,viongozi wa Serikali za mitaa na viongozi wa vyama vya waendesha Bodaboda katika Halmashauri ya Jiji la Tanga,
MKUU wa Polisi wilaya ya Tanga(OCD) Enock Ngonyani akizungumza wakati wa kikao hicho
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Madaraka Jijini Tanga Elizaberth Chawinga akizungumza wakati wa kikao hicho |
Sehemu ya wamiliki,waendesha bodaboda na bajaji,viongozi wa Serikali za mitaa na viongozi wa vyama vya waendesha Bodaboda katika Halmashauri ya Jiji la Tanga wakimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Henry Mwaibambe
Na Oscar Assenga,TANGAWAENDESHA Bodaboda Jijini Tanga wametakiwa kutii sheria na kutambua kuwa shughuli wanayoifanya ni halali kama ilivyo kwa kazi nyingine na kwamba kazi wanayoifanya siyo kama waganga wa kienyeji ambayo kila mmoja hutumia mtindo ‘Style’ ya aina yake katika kuagua.
Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Henry Mwaibambe alitoa Wito huo wakati akizungumza na wamiliki,waendesha bodaboda na bajaji,viongozi wa Serikali za mitaa na viongozi wa vyama vya waendesha Bodaboda katika Halmashauri ya Jiji la Tanga,
Katika kikao hicho kilicholenga,kukumbushana na kuelimishana juu ya umuhimu wa kuzingatia sheria za usalama barabarani na suala zima la ulinzi na Usalama Jijini Tanga,Kamanda Mwaibambe alisema Bodaboda na Bajaji wanapaswa kujitambua na kuzingatia Sheria.
Alisema kwamba, kazi hiyo ya Bodaboda inapaswa kufanywa kwa kuzingatia misingi ya sheria huku akiwataka ,kuzingatia suala la kufahamiana baada ya kuwa kila mmoja amesajiliwa katika Chama husika hatua ambayo itasaidia kudhibiti vitendo vya uhalifu kwenye Jiji hilo la Tanga,
“Usalama kwetu Bodaboda ndio kila kitu, mshirikiane vizuri na wenyeviti hawa wa mitaa, msikae na wahalifu kwenye vijiwe vyenu…”alisema Kamanda Mwaibambe huku akilaani tabia za baadhi ya Bodaboda kujihusisha na vitendo vya uporaji wa Simu na uhalifu mwingine.
Kamanda huyo wa Jeshi la Polisi Mkoani Tangaaliwataka waendesha bodaboda hao kujali maisha yao kwa kutokubali kutumbukia kwenye vitendo vya uhalifu kwa maelezo kuwa wako wanaoingia bila kujua na hata pale wanapobaini wamekuwa wazito katika kutoa taarifa.
“ Tuishi maisha ya kufahamiana, tujali maisha yetu tunapokutana na mtu hatu muelewi kwenye vituo vyetu tuone taarifa. Uporaji Simu imekuwa ni changamoto hivyo tufahamiane na Tanga tuna deni kubwa kuendelea kudumisha amani na usalama”alisema SACP Henry Mwaibambe.
SACP Henry Mwaibambe amewaasa waendesha bodaboda ba bajaji hao kutohusika katika kusafirisha madawa ya kulevya kama vile Mirungi, Bangi n ahata wahamiaji haramu na kwamba ikitokea vyombo vyao vikikamatwa kuhusika na matukio hayo ni Dhahiri kuwa vitataifishwa.
Amewataka wajasiriamali hao kujitahidi kuwa wakweli ili kuiwezesha Tanga kuzidi kustawina kwamba wawe tayari kumfichua yeyote yule atakayekwenda kinyume huku akiahidi kusdhirikiana na kila mmoja kwa maelezo kuwa milango ya ofisi yake iko wazi muda wote.
Awali katika kikao hicho Uongozi wa Bodaboda ulieleza kuwa kuna changamoto ubebaji wanafunzi zaidi ya wanne kwenye vyombo hivyo vya usafiri jambo ambalo ni hatari kwa usalama kero ambayo ilidaiwa kuchangiwa na wasafirishaji hao ikiwa ni pamoja na wazazi.
Katika hoja hiyo Zakaria Bernard ambaye ni Mkuu wa Operesheni za Jeshi la Polisi Mkoani Tanga alisema, hali ngumu ya maisha isiwe kisingizio cha waendesha bodaboda ama wazazi kuruhusu watoto wao ambao ni wanafunzi kupakizwa mshikaki kwenye vyombo vya usafiri.
Aidha waendesha bodaboda na bajaji walilalamikia kufanyiwa vurugu na madereva wa Hiace pindi wanapotaka kupakia abiria jambo ambalo limesababisha jamii hizo kupigana mara kwa mara ambapo wameliomba Jeshi la Polisi kuingilia kati ili kulipatia ufumbuzi suala hilo.
Changamoto nyingine waliieleza kuwa ni waendesha bodaboda kupigwa faini nyingi,kukamatwa kwenye maeneo yenye kona ambapo Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga SACP Henry Mwaibambe alisema amezichukua kero zote hizo huku akiahidi kwamba atazifanyia kazi.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Tanga, Abel Nyalecha aliwataka Wenyeviti wa mitaa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria waendesha bodaboda ambao wanapasua bomba za pikipiki makusudi ili kupiga kelele.
Alisema kwamba, wenyeviti hao wanaweza kuwasiliana na Jeshi la Polisi pindi yanapotokea matukio ya aina hiyo ambayo husababisha vurugu kubwa miongoni mwa jamii akisema kwamba viongozi hao wanahusika katika kulinda usalama huku wakishirikiana kwa karibu na jeshi hilo.
Post a Comment