WACHIMBAJI TANZANIA WAPATA SHILINGI BILIONI 3.6 ZA KUANZISHA BENKI YAO
Na Mwandishi wetu, Arusha
SHIRIKISHO la vyama vya wachimbaji madini Tanzania (FEMATA) kupitia wachimbaji wazawa wamechanga kiasi cha shilingi bilini 3.6 kwa lengo la kuanzisha benki yao itakayowawezesha kuwapa mtaji wa kuchimba madini.
Akitangaza kwa waandishi wa habari matokeo ya michango ya wachimbaji hao jijini Arusha, Mbunge wa Geita vijijini Joseph Musukuma (CCM) aliwapongeza wachimbaji hao wazawa kwa kuchanga fedha hizo.
Musukuma ambaye amewawakilisha wabunge wanaotoka maeneo yenye madini amesema uanzishwaji wa benki hiyo ni wazo lililotoka kwa mchimbaji wa dhahabu Baraka Ezekiel.
"Nitahakikisha tunamshawishi Rais Samia Suluhu Hassan ili aongoze harambee ya kukusanya fedha za uanzishwaji wa benki hii ya wachimbaji wa madini," amesema Musukuma.
Rais wa shirikisho la vyama vya wachimbaji madini Tanzania (FEMATA) John Bina amesema uanzishwaji wa benki hiyo utajibu changamoto mbalimbali za wachimbaji na wadau wote wanaonufaika na mnyororo wa thamani ya madini.
Bina ametaja wanufaika wa benki hiyo ni wachimbaji madini wakiwemo wamiliki wa leseni, wenye mialo, wenye migodi, miduara, wachenjuaji, wanunuzi wa magonga ya Tanzanite, wanunuzi wakubwa, wakati na wachuuzi.
"Mchakato wa uanzishwaji benki ya wachimbaji unahitaji maoni, uzoefu na utaalam ili kujiweka tayari hasa kununua hisa pindi benki hiyo ikianza kufanya kazi," amesema Bina.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la madini la Taifa (STAMICO) Dkt Venance Mwasse amesema uanzishwaji wa benki hiyo ni maendeleo makubwa na umuhimu hasa kwa wachimbaji wadogo nchini kwani wengi wao hawana mitaji.
Dkt Mwasse amesema wazo la uanzishaji wa benki ni zuri kwani hata mataifa mengine ya nje yataiga kwao na wametegua mtego mkubwa wa kuwa na benki ya wachimbaji.
"Mtaona fahari kuwa hata sisi wachimbaji wadogo tunaongeza mtaji wa nchi katika mapato kwa kuwa na benki kwani uchumi mkubwa ulioendelea ni ule uliopo katika mfumo wa benki," amesema Dkt Mwasse.
Mchimbaji wa madini ya dhahabu, Baraka Ezekiel kutoka mkoa wa Geita aliyeanzisha wazo la wachimbaji kuwa na benki amesema wachimbaji wanapaswa kuchangia kwanza kwani ni mali yao.
Mchimbaji maarufu wa madini ya Tanzanite, Bilionea Saniniu Laizer alisema uwepo wa benki hiyo itakuwa fursa kubwa kwa wachimbaji wadogo kwani wengi wao hawana mitaji ya kuchimba.
Makamu Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini mkoa wa Manyara (MAREMA) Money Yusuf amesema uwepo wa benki hiyo utaongezewa nguvu na ushirika kwa wachimbaji ili wawe na uchumi imara.
Mchimbaji wa madini ya Tanzanite Samweli Rugemaliza amesema wachimbaji wachange fedha nyingi kwani kila fedha atakazochangia kwenye benki hiyo ndiyo hisa atakazo miliki katika benki yao.
Mchimbaji wa madini ya ujenzi Doyo Hassan Doyo amewapongeza viongozi wa FEMATA kwa kufanyia kazi wazo zuri lililotolewa na mchimbaji mwenzao.

Post a Comment