Header Ads

test

KLABU YA GOFU JWTZ LUGALO YAWABURUZA DAR ES SALAAM GYMKHANA  "CRDB INTER CLUB CHAMPIONSHIP 2023"

Na.Khadija Seif,Michuzi TV

Klabu Ya Jeshi La Ulinzi La Wananchi Wa Tanzania-JWTZ Lugalo Gofu Imeibuka Kinara Katika Shindano La "CRDB INTER CLUB CHAMPIONSHIP 2023 "Lililofanyika Jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya kupokea kikombe Mwenyekiti Wa Klabu ya Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo amewapongeza wachezaji na kusema ni mwanzo wa Maandalizi ya Timu inayotarajia kushiriki Mashindano ya Dunia ya Majeshi mwisho Wa Mwaka huu.

"Ukiangalia mantiki nzima ya mchezo huu sio Kushindana Vilabu hivi viwili kinachotutofautisha ni majina tu ya vilabu lakini wachezaji ni walewale tu na hii yote ni kwa sababu ya kuongezeka kwa wachezaji wengi inapelekea kugawanyika kwa sehemu za kucheza mchezo wa gofu ila sote ni wa moja".


Aidha,Luwongo akatumia fursa ya kuwapongeza wachezaji kutoka klabu ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ) Daudi Isihaka pamoja Michael Massawe kwa kuleta Ushindi katika Mashindano ya Inspire Africa Golf Open 2023 yaliyofanyika Jijini Arusha .

Lugalo Imeibuka washindi baada ya Timu zake 14 kuibuka Na ushindi Kati ya timu 23 zilizoshiriki huku Dar Es Salaam GYMKHANA wakiambulia ushindi Kwa Timu tisa.

Kwa upande wake Mwenyekiti Chama Cha Gofu Tanzania TGU Gilman Kasiga aliyekuwa Mgeni Rasmi amepongeza ubunifu ulioonyeshwa Na VIlabu hivyo pia ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hasan Kwa Ujenzi Wa Uwanja wa Gofu Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

"Nimetumaini yangu kuwa kufanya hivyo ni kiashiria tosha kuwa anaipa taarifa Mamlaka na wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kushiriki katika mchezo wa gofu kutokana na yeye kuupa nafasi kupitia kiwanja hicho kilichojengwa"

Hata hivyo ameeleza sababu hasa kufanyika kwa shindano hilo na Malengo ambayo chama cha gofu (TLGU) inatamani kuyafikia kwa siku za usoni.

"Tulipokubaliana kuanzisha shindano hili tulikua tunalenga mchezo huu kuona unakuwa kwa kasi zaidi na unaleta ushindani hivyo chama chetu kitaendelea kuunga mkono wadau mbalimbali wenye nia ya dhati ya kuona mchezo huu unapewa nafasi kubwa kwenye jamii na hasa Sekta ya Michezo."

Hata hivyo Kasiga ameeleza kuwa kupitia chama chake wameonea Shindano hili liwe la Kimataifa na kuhusisha washiriki kutoka Mataifa mbalimbali.

Nae upande wake mdhamini wa shindano hilo Mkurugenzi wateja wakubwa kutoka Benki ya CRDB Prosper Nambaya amesema wataendelea kuunga mkono mchezo wa gofu kwa kuhakikisha shindano hilo linafanyika kila mwaka kwa kushirikisha vilabu hivyo vyenye mchango mkubwa katika mchezo wa gofu nchini.

"Benki yetu imekuwa ikitoa mchango kwenye jamii hususani upande wa Michezo mbalimbali ikiwemo Marathon, mpira wa Miguu lakini safari hii tumeamua kuingia kwenye mchezo wa gofu na tunategemea shindano hili kulifanya liwe kubwa kwa mwaka 2024.

Hata hivyo amesema CRDB watatoa ushirikiano mkubwa kwa timu ya watoto (Juniors) kwa kuhakikisha wanafikia malengo yao na kuwa wachezaji wa Kimataifa.
Mwenyekiti Wa Klabu ya Lugalo gofu Mstaafu Michael Luwongo akipokea Kikombe cha ushindi,Kushoto kwake Mkurugenzi wateja wakubwa kutoka Benki ya CRDB Prosper Nambaya , Kushoto Gilman Kasiga Mwenyekiti Chama Cha Golf Tanzania (TLGU) mara baada ya Kumalizika kwa Mashindano ya "CRDB INTER CLUB CHAMPIONSHIP " yaliyoshirikisha vilabu viwili Lugalo Gofu Pamoja na Dar Gymkhana yaliyofanyika katika Viwanja vya Gofu Lugalo Jijini Dar es salaam

No comments