MARIAM ULEGA AMPONGEZA RAIS SAMIA KUZIHAMASISHA YANGA, SIMBA MICHUANO KIMATAIFA
Na Mwandishi Wetu Mchuzi TV.
MJUMBE wa Baraza Kuu ya Jumuiya ya Wanawake Tanzania(UWT) kutoka Mkoa wa Pwani Mariam Ulega amempongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan Samia kwa kuweza kutoa hamasa kwa timu za Simba na Yanga katika mashindano yao ya kimataifa.
Mariam amesema hayo jana jioni wakati wa mapokezi ya timu ya Yanga ambayo imetoka kucheza fainali za Kombe la Shirikisho nchini Algeria na kufanikiwa kushika nafasi ya pili ambayo imewawezesha kupewa medali.
"Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa katika hamasa amehamasisha mpaka amenunua magoli kwa milioni 20 kwa hiyo tunampongeza sana sana, " amesema.
Amefafanua UWT Taifa wameungana na Mwenyekiti wao Mary Chatanda ambae naye ameungana na Rais katika hamasa hiyo kubwa kwa kusafiri na timu mpaka Algeria, hivyo wameamua kumpokea ili kuendelea kupitia timu moyo.
"Mimi ni Simba lakini ni muhimu kuwapongeza watani zangu wa jadi Yanga kwani kitendo cha kucheza na kufika fainali sio jambo dogo, " amesema.
Ameongeza kufika tu fainali wanahitaji kupongezwa kwani wameshindwa kuchukua kombe kutokana na kanuni kwani hawajafungwa huku akitoa mwito kwa watanzania kuwa na utamaduni wa kupongezana na kuacha kuonekana wivu.
Post a Comment