Header Ads

test

NMB WAZINDUA KAMPENI YA BONGE LA MPANGO MBINGA

MKUU wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma
Mheshimiwa Aziza Mangosongo amezindua kampeni ya
Bonge la mpango Kanda ya kusini inayotekelezwa na
Benki ya NMB.

Akizungumza kabla ya uzinduzi huo uliofanyika ndani ya
stendi ya mabasi mjini Mbinga, Mwakilishi wa Meneja wa
NMB Kanda ya Kusini Roman Degeleki amesema katika
kampeni hiyo zaidi ya shilingi milioni 260 zitatolewa kama
zawadi kwa washindi zaidi ya 100.

“kampeni hii itaendeshwa ndani ya wiki 12 kila wiki
washindi 12 watapokea shilingi laki moja kila
mmoja.mshindi mmoja atajipatia shilingi 200,000 na
mshindi mmoja atajishindia pikipiki”,alisema Degeleki.

Ameongeza kuwa katika kampeni hiyo washindi watano
watajinyakulia shilingi milioni moja kila Mwisho wa mwezi.

Hata hivyo amesema katika kuhitimisha kampeni
hiyo,washindi 11 watajishindia pikipiki,washindi watano
watajishindia bajaj na wengine saba watajishindia vifaa
vya kieletroniki.

Machi 29 mwaka huu benki ya NMB ilizindua kampeni
maalum yenye makusudi ya kurejesha faida kwa wateja
pamoja na kuhamasisha wa kujiwekea akiba kwa
watanzania ambapo hadi sasa wateja wa NMB zaidi ya 70
wamejinyakulia zawadi mbalimbali.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo mgeni rasmi Mkuu wa
Wilaya ya Mbinga Mheshimiwa Aziza Mangosongo
ametoa rai kwa watanzania kujenga utamaduni wa
kuweka akiba kwa kufungua akaunti katika benki ya NMB.


“Ukiweka akiba benki utakuwa na pa kukimbilia ukipata
changamoto kwa sababu shida haipigi hodi “,alisisitiza
Mangasongo.

Oscar Makwaya ni Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha
Ushirika Linda Wilaya ya Mbinga,akizungumza baada ya
uzinduzi huo ameipongeza NMB kwa huduma bora za
kifedha hali iliyosababisha wakulima wengi katika kijiji cha
Linda kufungua akaunti kwenye Benki hiyo
Uzinduzi wa kampeni hiyo ya NMB Bonge la mpango
kanda ya kusini yenye mikoa ya Ruvuma,Lindi na Mtwara
umefanyika mjini Mbinga.
Wateja wa NMB Tawi la Mbinga na baadhi ya wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa NMB Bonge la Mpango kwenye viwanja vya kituo cha mabasi mjini Mbinga
Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mheshimiwa Aziza Mangasongo akiinua bendera kuashiri uzinduzi wa NMB Bonge la Mpango Kanda ya kusini mjini Mbinga kushoto kwake ni Mwakilishi wa Meneja wa NMB Kanda ya kusini Roman Degeleki
Mwakilishi wa Meneja wa NMB Kanda ya kusini Roman Degeleki akizungumza mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya NMB bonge la mpango mjiini MbingaMkuu wa wilaya ya Mbinga Mheshimiwa Aziza Mangasongo akizungumza kabla ya kuzindua kampeni ya NMB Bonge la Mpang

No comments