POLISARIO WAADHIMISHA MIAKA 50 YA HARAKATI ZA UHURU, NCHI ZA AFRIKA ZIKO WAPI KUWATETEA?
Na Moses Ntandu, Auserd, Sahara Magharibi
Katika hali ya kushangaza sana Afrika ya leo bado kuna nchi mwanachama mwanzilishi wa Umoja wa Afrika nchi ya Sahara Magharibi bado inatawaliwa tena na taifa la kiafrika.
Penginge swali kubwa hapa ni jitihada zipi zonazochukuliwa na nchi za Kiafrika na ni nini kinafanyika kama juhudi au sauti moja kwa ndugu zetu wa Sahara Magharibi wanaoteseka jangwani wakati rasilimali zao zipo na ardhi yenye rutuba kubwa ikichukuliwa na nchi nyingine ya Kiafrika?
Je, viongozi wetu wa zamani kama Mwl Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania, Kwame Nkruma wa Ghana, Ahmed Ben Bella wa Algeria, Nelson Mandela wa Afrika Kusini na wengineo wengi waliokuwa wapigania uhuru wa Afrika ikiwa watainuka sasa...
Na kukuta kwamba nchi mwanachama wa Umoja wa Afrika anatawaliwa na mwafrika mwingine ni aibu kubwa sana hata kwa mabara meingine njevya Afrika yanaposhuhudia hali hii ikiendelea barani kwetu.
Maswali mengine mengi lazima yawe akilini mwetu waafrika bila kujali nyadhifa na mamlaka zetu.Kinachotokea hapa Sahara Magharibi ni ukatili na ukiukwaji wa haki za wanaSahara Magharibi.
Hilo linapaswa kulaaniwa na kukemewa na wapenda amani duniani kote na kwa bara letu ni aibu kubwa na ni lazima ilaaniwe kwa njia yoyote ile na watu wote wanaotakia heri bara letu na Afrika.
Hili jambo baya zaidi kushuhudiwa katika karne hii ya 21 barani Afrika na ni makosa ya ukoloni ndani ya bara moja. Sahara Magharibi kutawaliwa ni suala la aibu kwa bara la Afrika
Inasikitisha sana kuona nchi ya kiafrika ikiinyonya na kuitawala nchi nyingine hapa barani Afrika badala ya kumsaidia na kumpa mkono wa kumsaidia. Hii ni aibu na ni zaidi ya unyama.
Kinachoendelea katika ardhi ya Sahara Magharibi ni uhalifu dhidi ya ubinadamu na nchi zote za Kiafrika, mashirika ya kimataifa na nchi nyingine za nje ya Afrika hazina budi kupaza sauti kuunga mkono koloni hili la mwisho la Afrika kuwa huru.
Sahara Magharibi kama taifa barani Afrika na mwanachama mwanzilishi wa Umoja wa Afrika bado inatawaliwa bila kujali juhudi nyingi zilizofanywa ili kuwa huru lakini bado eneo lao linakaliwa kimabavu.
Hivi karibuni Chama cha kupigania uhuru wa Sahara Magharibi cha Polisario Front Movement kiliadhimisha miaka 50 ya harakati za kupigania uhuru wao.
Katika sherehe kubwa hizo zilizofanyika katika mji wa Auserd Sahara Magharibi Rais wa Sahara Magharibi Brahim Ghali Katika hotuba yake alieleza mwanzo wa chama hicho na harakati zao hadi kufikia miaka 50 sasa.
Ghali alieleza harakati za kuanzishwa kwa kundi la Polisario Front na kuzuka kwa mapambano ya silaha dhidi ya ukoloni wa Uhispania na mnyakuzi wa Morocco.
Rais Ghali alieleza kwamba "Algeria na Rais wake Abdelmadjid Tebboune, wamethibitisha msimamo wao kwa kuwiana kabisa na katiba na maazimio ya Umoja wa Mataifa na Sheria ya Katiba ya Umoja wa Afrika na hasa kwa kanuni na maadili ya mapinduzi matukufu ya Novemba mosi 1954. Shukrani zangu na shukrani kwa watu wa Algeria."
Pia alisifu bara la Afrika, watu wake na mataifa yake ambayo yamezingatia nia ya Sahrawi kama sababu ya haki ya Kiafrika. Pia alitoa salamu kwa vyama vyote vya ukombozi wa Afrika "ambao mapambano yao ya ukombozi wa Afrika kutoka kwa aina zote za ukoloni yanatuunganisha". Alisema
Katika hafla ya kuadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa kwa kundi la Polisario Front na kuzuka kwa mapambano ya silaha, mamlaka ya Sahrawi yaliandaa programu kubwa na tofauti.
Mbali na maonyesho ya kijeshi na ya kiraia, walifanya mikutano mingi yenye mada kadhaa mnamo Mei 20 na 21, pamoja na meza za pande zote zinazohusiana na suala la Sahrawi.
Mpango wa sikukuu pia ulijumuisha matukio yanayoangazia fikra za mwanamke wa Kisahrawi pamoja na maonyesho yaliyotolewa kwa vitabu vilivyoandikwa na waandishi wa Sahrawi.
Kwa upande mwingine mkuu wa mkoa wa Auserd Khira Bulahi aliwakaribisha wajumbe walioshiriki katika Kongamano hilo huku akipongeza mchango wao katika kusindikiza mapambano ya wana Saharawi na sababu zake za haki, huku akitoa wito wa kuongezwa kwa juhudi za kutetea Sahrawi duniani kote.
Mkutano wa Kimataifa wa Mshikamano na Wananchi wa Sahrawi unapania kuanzisha makundi ya mabunge ya mshikamano na wananchi wa Sahrawi ikiwa ni hatua itakayoimarisha diplomasia ya bunge katika nyanja zake mbalimbali.
Wakati huohuo gwaride la kijeshi lililoandaliwa wakati wa hafla hiyo ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa kwa kundi la Polisario Front na kuzuka kwa mapambano ya kijeshi ya Sahrawi lilitamalaki na kuonesha tukio hilo na matarajio ya Wasahrawi, na kufichua hasa kiwango cha juu cha taaluma na maandalizi mazuri ya vitengo vya jeshi la Sahrawi pamoja na uwezo wa kisasa zaidi wa vifaa na kijeshi.
Vikosi vya askari wa miguu vilivyofungua gwaride hilo vilitekeleza zoezi hilo la mpangilio mkali kwa ukamilifu kama askari wa miguu walio na mitambo, pamoja na vifaa vya huduma za afya, uhandisi na miundo ya forodha ilizindua silaha na vifaa vya juu.
Taaluma hiyo hiyo imeonyeshwa, kwa kiwango cha juu, na vitengo vya vikosi maalum. Vitengo vya wanawake wa kijeshi pia vilishiriki kwenye gwaride.
Taaluma nyingine iliyobainishwa katika kiwango cha uundaji tofauti ni usawa kati ya askari wa zamani na mambo ya vijana ambayo vilionyeshwa, kwa njia ya kisasa zaidi.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa wakati wa gwaride la kijeshi, vitengo vya jeshi la Sahrawi vinapata mafunzo makali zaidi ya kijeshi ili kuwa na ufanisi katika hali zote.
Rais wa Jamhuri na Katibu Mkuu wa Chama cha Polisario, Brahim Ghali, alisifu bidii na nia ya kushinda ambayo ni tabia ya vitengo vya jeshi la Sahrawi, akisisitiza kwamba ujuzi na ari hizo zimerithiwa kutoka kwa vizazi vikongwe vya viongozi kama El Wali Mustapha Sayed na Mohamed Abdelaziz.
Ikumbukwe kwamba mwezi September 2022 Mahakama ya Haki ya Umoja wa Ulaya ilitoa hukumu kwa Umoja wa Ulaya wa kuacha kutumia mikataba ya biashara na uvuvi na Morocco na kulikandamiza taifa la Sahara Magharibi.
29 Septemba 2021
Picha: Mwakilishi wa Polisario barani Ulaya, Oubi Bachir, akiwa na Manuel Devers kutoka timu ya wanasheria ya Polisario.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa kutoka kwa Mahakama hiyo ilieleza haswa kwamba Polisario ina uwezo wa kuwawakilisha watu wa Saharawi mbele ya mahakama za Ulaya.
Haki ya watu wa Saharawi kupata kibali haijaheshimiwa, mahakama ilisema. Pia ilisema kwamba Muungano haungeweza kuchukua nafasi ya "ridhaa" ya watu wa Saharawi kwa hoja ya "manufaa".
"Kwa kuzingatia dhana ya kisheria ya watu na ridhaa, "mashauriano ya watu walioathiriwa" yaliyoandaliwa na taasisi hayakuweza kusababisha kujieleza kwa ridhaa ya watu wa Saharawi", taarifa hiyo ilieleza, kwa ufafanuzi wa hukumu katika kesi namba T-344/19 na T-356/19 (kuhusu uvuvi) na Uamuzi wa kesi T-279/19 (kwenye biashara)
“Huu ni ushindi wa haki, na kwa watu wa Sahara Magharibi. Tunatumai kuwa Nchi Wanachama wa EU sasa hatimaye zitatii maamuzi ya Mahakama, na kuiondoa Sahara Magharibi kutoka kwa mawanda mapana ya mahusiano ya Muungano na Morocco.
"Ni wakati muafaka kwa EU kuacha kuwa sehemu ya tatizo katika koloni la mwisho barani Afrika, na kuwa sehemu ya suluhu”, alisema Sylvia Valentin, Mwenyekiti wa Sahara Magharibi katika shauri hilo
Mahakama ilifafanua kwa mara nyingine kwamba Sahara Magharibi haiwezi kuwa sehemu ya makubaliano na Morocco.
Chama tawala cha Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni mmoja wa wapigania uhuru na rafiki mkubwa wa ujumbe wa vuguvugu la Polisario, anayeunga mkono harakati za uhuru wa watu wa Sahara Magharibi. CCM ina historia nzuri ya ukombozi hasa karibu nchi zote za ukanda wa kusini mwa Afrika.
Hali kadhalika enzi za kupigania uhuru wa mataifa meingi ya Afrika Tanzania ilikuwa mstari wa mbele katika harakati hizo jambo ambalo linapaswa kiruthiwa na kizazi cha sasa na kusaidia harakati za Sahara Magharibi.
Hata chimbuko la jina Chama Cha Mapinduzi maana yake ni chama cha kuleta mapinduzi ya kujitawala na kuwa na amani na utulivu, Chama cha mapinduzi ambacho kililenga kulikomboa Bara la Afrika kutoka kwa nguvu za kikoloni kilifanikisha adhma yake kwa kiwango kikibwa mno.
Uungaji mkono wa Tanzania kwa Polisario ni historia kwa sababu ulikuwepo tangu wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika chini ya hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere ambaye kwa kiwango kikubwa alishirikiana na kiongozi wa Algeria rais Ahmed Ben Bella.
Mwaka jana Novemba 2022 Rais Brahimi Ghali alitembelea Tanzania na kuhudhuria Mkutano Mkuu wa CCM mjini Dodoma na kuhutubia mkutano huo ambapo aliomba kuimarishwa kwa ushirikiano wa CCM na Polisario.
Rais wa Sahara Magharibi Brahimi Ghali akihutubia katika hafla ya maadhimisho ya miaka50 ya Polisario

Pia alisisitiza na kuomba watanzania wote hasa kizazi cha sasa kukumbuka wosia wa baba wa taifa Mwl Nyerere wa kutetea wanyonge na kuunga mkono juhudi za kupigania uhuru wa Sahara Magharibi.

Post a Comment