Header Ads

test

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA TAASISI ZA KISAYANSI KUFANYA TAFITI ILI KUPATA MAJIBU YA KISAYANSI...

Na Janeth Raphael MichuziTv - Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum inaendelea kushirikiana na Taasisi za kisayansi nchini zinazofanya tafiti mbalimbali ili kupata Majibu ya kisayansi yanayowezesha kuleta suluhu za kuinua uzalishaji na vipato vya makundi Maalum.Akifungua Mafunzo ya utengenezaji wa Vijarida sera vitakavyotatua changamoto za Makundi Maalum, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu ameelezea ni namna gani Sayansi na teknolojia inaweza kutumika katika kusaidia kupata majawabu yenye ushahidi ili kusaidia makundi maalum.

Aidha amesema Mazingira yanaruhusu kuleta majawabu yenye ushahidi kwani miundo mbinu ipo na imesambaa nchini ikiwemo barabara, Nishati, taasisi binafsi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa idara ya Makundi Maalum kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Juma Samwel amesema Serikali inapambana kuhakikisha wafanya biashara ndogondogo wanakua kiuchumi.

“Tunatamani Makundi haya maalum yaweze kurahisishiwa mazingira ya kufanyia kazi kwa kushirikishwa kwa ukaribu katika masuala yanayowahusu lakini pia mamlaka husika na yanayowagusa wazalishaji hawa wadogo kufanya nao kazi kwa ukaribu ili kurahisisha uzalishaji wao kwa mfano Latra kuweza kuongeza ukaribu nao ikiwemo kuwaelemisha juu ya masuala mbalimbali”

Aidha, Mkurugenzi wa uratibu na uendelezaji wa Utafiti,Tume ya Sayansi na Utafiti (COSTECH) Dkt. Bugwesa Zabron Katale amesema lengo kubwa la taasisi ni kutatua changamoto zinazokumba Jamii katika kada mbalimbali.

“Lengo kubwa la Tume ya Sayansi na Utafiti ni kutatua changamoto zinazoikumba jamii kupitia tafiti mbalimbali na kuja na masuluhisho yatauowezesha kuleta mabadiliko na maendeleo katika Taifa.Hivo kuwa na Taifa linalofanya vitu kitaalam na si kwa mazoea”

No comments