Header Ads

test

WATU 18 WANUSURIKA KUFA BAADA YA GARI WALIYOKUWA WAKISAFIRIA KUPATA AJALI WILAYANI SAME

Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV-Same

WATU 18 waliokuwa safarini kutoka Dar es Salaam kwenda Arusha wamejeruhiwa  na kukimbizwa Hospitali ya Wilaya ya Same na tayari Sita kati yao wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa KCMC kwa matibabu baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupata ajali.

Akizungumza leo Julai 14, 2023,  Dk.Alfred Seti aliyekuwa zamu katika Hospitali ya Wilaya ya Same amesema  wamepokea jumla ya majeruhi 16 waliotokana na ajali hiyo na baada ya matibabu ya awali wamelazimika kuwahamisha Hospitali ya Rufaa KCMC majeruhi sita ambao wanahitaji  matibabu ya zaidi na 10 wanaendelea  kupata huduma.

Katika ajali hiyo iliyohusisha Toyota Coster yenye namba za Usajiri T819 DVD imedaiwa chanzo ni  uzembe wa dereva kutozingatia sheria na alama za barabara ambaye baada ya kutokea ajali hiyo ametokomea kusikojulikana.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni aliyefika kuwajulia hali majeruhi hao amewapa pole na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awaponye na warejee kwenye shughuli za ujenzi wa Taifa huku akiwataka pia madereva kuogeza umakini hasa wanapofika kwenye Wilaya hiyo.

Pia amewashauri abiria kuwa na tahadhari kutoa taarifa kufichua madereva ambao wamekuwa na tabia ya kukiuka sheria za usalama barabarani ili kuepusha madhara kama hayo.

Wakizungumza kwa shida baadhi ya majeruhi hao wamedai  chanzo ni uzembe wa dereva kutokuwa makini hata kabla ya ajali kukaidi alama za barabarani.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Same, watu 18 wamejeruhiwa katika ajali hiyo, wawili wanaendelea na matibabu kituo cha afya Hedaru, 16 walifikishwa Hopitali ya wilaya kati yao sita wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa KCMC Na 10 bado wanaendelea na matibabu Hospitalini hapo.

Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni akiwajulia hali baadhi ya majeruhi waliopata ajali katika gari waliyokuwa wakisafiria.

No comments