NIC Insurance imeendelea kulipa madai kwa wakati.
Na Mwandishi Wetu, Mbeya
NIC Insurance imekabidhi meli ya Mv. Mbeya II kwa Mamlaaka ya Bandari (TPA) baada kukamilika kwa matengenezo kufuatia hitilafu ya injini iliyosababishwa na dhoroba iliyotokea wakati Meli hiyo inakaribia kutia nanga katika Bandari ndogo ya Itungi (Kiwira) iliyopo Kyela jijini Mbeya.
Akizungumza mara baada ya Makabidhiano hayo Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Insurance Bw. Hardbert Polepole. amesema NIC inafanya kazi kwa vitendo katika kukidhi mahitaji ya mteja pale inapotokea janga.
"NIC Insurance imesimamia matengenezo ya meli ya MV. Mbeya II ikiwa ni takwa la mkataba wa bima kufidia uharibufu uliojitokeza" amesema Hardbert Polepole.
Baada ya matengenezo kukamilika, Meli hii ilifanyiwa ukaguzi ili kuthibitisha ubora wake na taasisi ya udhibiti wa vyombo vya majini (TASAC) ambapo Meli hiyo ilipewa cheti cha kukidhi viwango ubora hivyo kuruhusiwa kuendelea kufanya shughuli zake za usafirishaji.
NIC Insurance imelipa kiasi cha shilingi miliioni 390 kwa Mkandarasi Mantrack Tanzania LTD ili kukamilisha matengenezo ya injini ya meli hiyo jambo lililoletw tabasamu kwa Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe Josephine Manase kwa niaba ya wananchi wa maeneo yanayonufaika na usafiri huo.
"Tuna furaha kubwa kutokana na kurejea kwa huduma za usafiri wa abiria na mizigo ya meli ya Mv. Mbeya II ambayo itaendelea kuchochea shughuli za kiuchumi na jamii kwenye ukanda wa ziwa Nyasa.” Amesema Mhe. Josephine Manase.
Mhe. Josephine aliipongeza NIC Insurance kwa kuboresha huduma za bima hususan katika ulipaji wa madai kwa wakati jambo lililosababisha kukamilika kwa matengenezo ya Meli hiyo inayoenda kuboresha huduma ya usafiri na kuimalisha uchumi wa mtu mmoja mmoja, Wilaya ya Kyela na Taifa kwa ujumla.
NIC inawahakikishia wawekezaji na watumiaji wa Meli hii usalama wakati wowote waitumiapo.
Aidha Manase ameipongeza NIC kwakuchaguliwa Superbrands Afrika Mashariki hivyo waendelee kuwa mfano katika kufanya kazi kwa bidii, weledi na ufanisi mkubwa katika kuwahudumia wateja wake.
"Mteja akileta madai yanaenze kufanyiwa kazi mara moja kwani nimeambiwa ubora wa mifumo ya kidijitali mliyowekeza kwa gharama kubwa ni ya kisasa sana hivyo itendeeni haki." Amemalizia Mkuu huyo wa Wilaya.
Meli ya MV Mbeya II ikiwa katika safari baada ya Matengenezo ya NIC Insurance ambayo ilipata hitilafu wakato ikitega nanga katika Bandari , Kyela mkoani Mbeya.
Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NIC akizungumza na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Insurance Hardbet Polepole (Katikati) mara baada ya kukabidhi Meli ya MV Mbeya II Bandarini , Kyela mkoani Mbeya
Mkuu wa Wilaya ya kyela Josephine Manase (Mwenye Nguo ya Kitenge) akizungumza mara baada ya kushuka katika Meli ya Mbeya II Watendaji wa NIC Insurance iliyotengenezwa na kufanyiwa Maboresho kutoka na Bima waliokata baada ya kupata hitilafu wakati wa kutega Nanga
Post a Comment