WAZIRI NAPE AZINDUA SHAHADA YA MEDIA ANUWAI NA MAWASILIANO KWA UMMA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA (IAA)
Leo Julai 20, 2023, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) amezindua Shahada ya ya Media Anuwai na Mawasiliano kwa Umma katika Chuo cha Uhasibu Arusha.
Kupitia hafla hiyo Waziri Nape amesema kuwa uzalishaji na ulaji wa maudhui ya vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii katika kipindi hiki cha Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia unategemea sana Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa kuwa TEHAMA ndio msingi wa Media Anuwai, hivyo uamuzi wa kuunganishwa kwa Media Anuwai na Mawasiliano kwa Umma ni uamuzi sahihi.
Pia Waziri Nape amesema kuwa Tasnia ya Habari na Mawasiliano inahitaji watu mahiri wenye weledi watakao kuwa daraja la kuunganisha jamii na Serikali. Vyombo vya habari dhabiti hutathmini, huchanganua na kuanzisha mijadala inayochochea kupatikana kwa utatuzi wa changamoto mbalimbali za jamii na utambulisho chanya wa nchi Kimataifa.
Sambamba na hayo Waziri Nape ametoa rai kwa wamiliki wa vyombo vya habari kutoa fursa kwa wanafunzi hao kupata nafasi ya kufanya mazoezi katika vyombo mbalimbali vya habari vya jijini Arusha ili waweze kufanya mazoezi kwa vitendo ili kufahamu uhalisia wa mazingira ya kazi zao na kupata uzoefu.
Naye Mkuu wa Chuo hiko, Prof. Eliamani Sedoyeka amesema kuwa kwa kuzangatia mabadiliko makubwa ya TEHAMA chuo hiki kimeona ipo haja ya kuanzisha shahada hiyo ili kuweze kuwa na wataalam wanaoweza kuchakata taarifa zenye weledi na zinazoendana na maendeleo hayo ya TEHAMA.
Post a Comment