Header Ads

test

MJUMBE UWT TAIFA MARIAM ULEGA AHIMIZA MSHIKAMANO KWA WANAWAKE

Na Mwaandishi wetu  Kibaha

MJUMBE wa Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mariam Ulega amewataka wanawake wilayani  Kibaha mkoani Pwani kudumisha mshikamano ndani na nje ya jumuiya hiyo ili kuweza kusaidia jamii.

Mariam Ulega ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la UWT Taifa ametoa kauli hiyo  alipokuwa akizungumza na wanawake wa Kata ya Kibaha  wakati wa mkutano mkuu wa jumuiya hiyo.

"Wanawake tunapokuwa na mshikamano tutalisaidia Taifa letu kwenye nyanja mbalimbali  na hasa za ukuaji wa uchumi wetu, " amesema Mariam Ulega.

Aidha amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ambavyo amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha maendeleo ya Taifa letu yanazidi kukua.Amekuwa kiongozi wa mfano na mwenye kuigwa katika Taifa letu.

Pia katika mkutano huo Mjumbe huyo amewaunga mkono wanawake wa kata hiyo kwa kuwachangia kiasi cha Shilingi Milioni mbili ili ziweze kuwasaidia katika kukuza mtaji wao.

Amewasisitiza viongozi wa jumuiya kuendelea kushuka chini kwa jamii ili kusikiliza changamoto zinazowakabili kama vile wanavyofanya viongozi wetu wa kitaifa Mama Chatanda  na Makamu wake Mama Shomari.

"Rais wetu kafanya mambo mengi na ya kuonekana kwa Watanzania hivyo hatuma wasiwasi na kura kwani mengi yanaonekana ambayo Mama Samia Suluhu Hassan ameyafanya kwa ufanisi wa hali ya juu, "amesema Mariam Ulega 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Kata ya Kibaha Mama Mahelo amemsifu Mjumbe wa baraza hilo Taifa kwa maneno yenye hekima kwa Wanawake wa Kibaha na Pwani kwa ujumla.
Mjumbe wa Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mariam Ulega akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa jumuiya hiyo Kibaha mkoa wa Pwani.
Mjumbe wa Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mariam Ulega (kulia) akiteta jambo na wanachama wa (CCM)
 

No comments