WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.
Selemani Jafo ametoa rai kwa wakuu wa mikoa kuifanya ajenda ya usafi wa
mazingira kuwa ya kudumu.
Ametoa wito huo tarehe 26 Agosti, 2023 wakati akizungumza wakati wa
Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa
yanayofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha
mkoani Pwani.
Dkt. Jafo amewataka wakuu hao wa mikoa kuzielekeza Mamlaka za Serikali za
Mitaa zilizo chini yao kusimamia vyema zoezi la usafi wa mazingira katika
maeneo yao ili kuifanya miji kuwa safi.
Alisisitiza kuwepo na utaratibu maalumu wa kujisaidia (kuchimba dawa) kwa
abiria wanaosafiri kwa mabasi badala ya porini kama unavyofanyika kwa
baadhi ya mabasi hali inayosababisha uchafuzi wa mazingira.
Aidha, Waziri Jafo aliwataka wakuu wa mikoa hao kusimamia suala la upangaji
wa miji katika maeneo yao ili uwekezaji usikwame kutokana na changamoto
za kimazingira.
Alisema kuwa bila kupanga miji vizuri uwekezaji unakuwa ni changamoto
kubwa kwani itawalazima wawekezaji kusubiri kupata Cheti cha Tathmini ya
Athari kwa Mazingira (EIA) kabla ya kuanza hatua ya ujenzi wa miradi.
“Mtu atataka kujenga kiwanda katika makazi ya watu, mambo yanakuwa
yanaingiliana na mwisho wa siku wakati mwingine EIA zinachelewa kwasababu
tumeshindwa kufuata utaratibu wa mipango miji hivyo, tuwasisitize watu wetu
wa mipango miji kuhakikisha wanapanga vizuri miji yetu kwa kushirikiana na
Wizara ya Ardhi,” alisisitiza.
Kwa upande mwingine Waziri Dkt. Jafo aliwahimiza viongozi hao kuendelea
kusimamia zoezi la upandaji wa miti milioni 1.5 kwa mwaka katika kila
halmashauri wanazozisimamia ili hifahi ya mazingira iwe endelevu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza
wakati wa Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa
Mikoa yanayofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere – Kibaha
Mkoa wa Pwani tarehe 26 Agosti, 2023.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)

Post a Comment