Header Ads

test

Gavana BOT ampongeza Rais Samia kwa Royal Tour.

Na Mary Margwe, Geita

KATIBU Mkuu,Wizara ya Habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo wa Zanzibar Fatma Hamad Rajab amewaasa Wanawake wachimbaji ( TAWOMA ) kuhakikisha kuwa changamoto wanazokutana nazo katika shughuli zao wanazichukulia kama fursa, huku akiwataka kuhakikisha wanasambaza elimu ya uchimbaji kwa vijana hususani wa kike ili waweze kujitegemea na kumudu mahitaji katika familia.

Fatma Rajab ameyasema hayo Jana alipotembeea katika banda la Chama cha Wachimbaji Madini Wanawake (TAWOMA) katika maonesho ya Madini yanayoendeea katika viwanja vya Bombambii katika mji wa Geita mkoani Geita, ambapo amewataka pia kuhakikisha wanasambaza elimu ya uchimbaji kwa vijana hususan wa kike ili waweze kujitegemea na kumudu mahitaji katika familia.

“ Wanawake Leo mna jambo lenu sio, Sasa naomba tuhakikishe kuwa changamoto mnazokutana nazo katika shughuli zenu mnapaswa mzichukulie kama fursa ,lakini pia muendelee kutoa taaluma hasa kwa vijana wa kike kwa sababu wao ndiyo wahitaji zaidi ili mwisho wa siku waweze kupambana wenyewe kuhudumia familia badala ya kuwategemea wanaume" amesema Katibu Mkuu huyo.

“Hakikisheni wanawake wenzangu mnajitahidi kuonyesha ujasiri, kupambana na kuonyesha wanawake tunaweza bila kumtegemea mwanaume,tufuate mfano mzuri wa Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye anaonyesha kwa vitendo kwamba wanawake tunaweza, na atakayebisha hilo huyo atakuwa ana chuki zake binafsi.”amesisitiza Rajab

Awali Katibu wa TAWOMA Salma Ernest ameelezea mafanikio ya chama hicho katia kipindi cha miaka miwili ya Rais Samia huku akisema,chama kimeweza kufanya programu mbalimbali za kujikwamua kiuchumi kupitia sekta ya Madini.

Amesema,chama hicho kina wanachama mikoa 21 ya Tanzania na wanatarajia kuongeza mikoa mingine lakini pia wapo katika wilaya 41 na wana matawi au programu ya vijana ambao mpaka sasa wana vikundi 14 vya vijana ambao wamejiajiri kwa kutengeneza vitu mbalimbali kwa kutumia madini yenye ubora wa chini ambayo hayana soko.

Aidha amesema,chama hicho kinaendesha vikundi 34 vya kusaidia jamii ambapo 17 vipo Tanga na 12 kutoka Morogoro vijijini ambavyo hukopeshana na hivyo kumudu kusaidia familia .

Katika hatua nyingine amesema chama hicho kinatimiza miaka 25 ya chama chao na wamekuja na programu iitwayo Malkia wa Madini ambapo wameandaa programu migodini pamoja na afya ya mama na mtotom,utunzaji umbuumbu ,eimu ya miopo,vifaa na tenoojia ambapo pia wameungana na maundi maaum waemavu ambao wapo nao wenye programu hiyo.

Amesema,Sherehe hizo zitafanyika Septemba 29 mwaka huu ambapo watakuwa na matembezi ya Hisani kutoka ukumbi wa Halmashauri mpaka kwenye viwanja vya maonesho huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Maendeeo ya Jamii,Jinsia na Maundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima huku uzinduzi wa proramu hiyo ukipangwa kutafanyia Otoba 30 .

Katika sherehe hizo mgeni rasmi atazindua na kumvisha taji malkia wa Madini Tanzania 2023









No comments