MWENYEKITI WA WACHIMBAJI WADOGO NYANG’HWALE ASISITIZA VIONGOZI WA DINI KULIOMBEA TAIFA.
Na Nasra Ismail, Geita
Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji wadogo wa madini Wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita,Misana Nyabange amewataka viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa libaki kuwa na amani pamoja na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani .

Misana ametoa wito huo wakati akiwa mgeni rasmi kwenye Harambe ya umaliziaji ujenzi wa Kanisa la AICT Ufunuo lililopo Mkoani Shinyanga.
Misana amesema wajibu mkubwa ambao viongozi wa dini wanao kwa sasa ni kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kuliombea Taifa na kuombea amani iendelee kudumu nchini na watanzania waendelee kuwa wamoja na kushikamana katika shughuli za kujiletea maendeleo.
“Ndugu zangu waumini wa Kanisa la AICT Ufunuo pamoja na kwamba leo nashiriki katika shughuli ya kuwezesha umaliziaji wa kanisa letu lakini nitumie fursa hii kuwaomba muendele kusisitiza amani na upendo kwa waumini wenu na pia kuliombea Taifa tumuombe Rais wetu najua anania ya dhati ya kuwatumikia watanzania lakini shetani naye yupo Kazini wakati mwingine amekuwa akijaribu kutaka kuondoa amani ya Taifa”Misana Nyabange Mwenyekiti wa Wachimbaji wadogo Wilaya ya Nyang’hwale.
Aidha Mbali na kutoa Nasaha pia amewawakilisha kiasi cha Sh,Milioni moja na laki sita na akihaidi kutoa kiasi cha sh,Milioni moja mwanzoni mwa Mwanzoni mwa mwezi wa 10 kwaajili ya ujenzi wa Kanisa la AICT Ufunuo Shinyanga.

Katika harambe Hiyo kiasi cha Sh,milioni 7 zimepatikana ambazo zitasaidia kuezeka kanisa hilo ambalo litakuwa na uwezo wa kubeba waumini zaidi ya 1000.
Post a Comment