Header Ads

test

SERIKALI KUBORESHA MAZINGIRA KADA YA USTAWI WA AAMII

Na WMJJWM Dodoma

Serikali itaendelea kuboresha mazingira, miundombinu na Huduma kwa Maafisa Ustawi wa Jamii ili wafanye kazi kwa ufanisi.

Akifunga mkutano wa mwaka wa kiutendaji wa Maafisa Ustawi wa Jamii, Septemba 7, 2023 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amesema Maafisa hao wana dhamana kubwa kuhakikisha usalama na amani ndani ya jamii.

"Ajenda hii ni muhimu na imebebwa kwa uzito na viongozi wetu wa kitaifa hususani Mhe. Samia Suluhu Hassan, ndio maana aliunda Wizara hii kwa sababu anajua changamoto, malengo, matatizo ya Watanzania hivyo Maafisa mliopo hapa mtakuwa mabalozi wazuri kwa wananchi, muwapokee, mtatue matatizo yao, wajue kwamba Serikali yao ipo inafanya kazi." amesema Mhe. Mwanaidi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Seif Shekalaghe amesema Maafisa Ustawi wa Jamii ni muhimu sana kwa jamii kwani matatizo mengi yanayotokea hasa ukatili wa kijinsia yanatokana na uwepo wa matatizo ya kisaikolojia hasa Afya ya akili.

"Sisi Makatibu Wakuu na ninyi Maafisa Ustawi wa Jamii ndio watekelezaji wa mambo yote kwa wananchi naamini tukionesha mshikamano nawahakikishia kuwa malengo yetu ya kuwahudumia wananchi yatakuwa yametimia" alisema Dkt. Shekalaghe

Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI (Afya) Dkt. Wilson Charles amewaambia Maafisa Ustawi wa Jamii hao kuwa Ofisi hiyo itashirikiana na Mamlaka nyingine kuhakikisha inatatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo uhaba wa Maafisa na vitendea kazi katika kuwahudumia wananchi.

Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii umeshirikisha kutoka Wizara, Mikoa Halmashauri na Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi ukiwa na kauli mbiu isemayo: Malezi Makuzi na Afya Bora ya
 Akili ni Jukumu letu sote.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akizungumza na Maafisa Ustawi wa Jamii wakati akifunga Mkutano wa Mwaka wa Maafisa hao uliofanyika Septemba 06-07, 2023 jijini Dodoma.










No comments