JAJI MKUU AAGIZA KUANZISHWA KWA MAHAKAMA KUU GEITA
Na Nasra Ismail ,Geita
Jaji mkuu wa Tanzania na mwenyekiti wa tume ya utumishi wa Mahakama Profesa Ibrahimu Juma ameagiza kuanzishwa kwa mahakama kuu mkoani Geita, huku lengo likiwa ni kusogeza huduma za kimahakama kwa wananchi.
Akizungumza na wadau wa mahakama Jaji mkuu wa Tanzania wakati alipokuwa katika ziara ya siku mbili ya kuzungumza na watumishi wa mahakama mkoani Geita,ili kusikiliza changamoto na michango ya jinsi gani mahakama iboreshe huduma zake alisema kuwa mahakama hiyo itasaidia kuharakisha mashauri ili hukumu itolewe kwa wakati.
Aidha Profesa Ibrahimu Juma aliwataka watumishi na wadau wa wanaoshughulika na mfumo wa haki jinai kuisoma ripoti ya tathmini iliyofanywa na taasisi ya REPOA juu ya utendaji kazi wa mahakama nchini katika kutoa haki kwa wateja wao.
Taasisi huru ya repoa ilifanya Tafiti mwaka 2019 na kubaini kiwango cha utoaji haki kwa wananchi ulikuwa ni wa asilimia 78 lakini kwa sasa viwango hivyo vimepanda hadi asilimia 88 mwaka huu wananchi wamelidhishwa na mfumo wa utoaji haki ktk mahakama ,huku dhana ya rushwa mahakamani imepungua kutoka asilimia 8 2019 hadi 6 mwaka huu kwa Mahakam kuu.
Kwa upande mwingine Jaji alipata nafasi ya kutembelea jengo la mahakama ya Geita ambalo litatumika kwa muda kutoa huduma wakati mahakama kuu ikiendelea kusubilia jingo jipya la mahakama kuu ambalo litakalotumika na mahakama ya hakimu mkazi wilaya huku ile ya mwanzo ikipisha ili mahakama kuu iendelee kutoa huduma.
Post a Comment