Header Ads

test

Waziri Simbachawene amewataka maafisa utumishi kusimamia sera pamoja na kuzingatia sheria

Na. Vero Ignatus, Arusha

Waziri wa nchi,ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh George Simbachawene amewataka maafisa utumishi kuendelea kusimamia sera pamoja na kuzingatia sheria na taratibu za uwajibikaji na maadili katika utendaji kazi wao.
Mh Simbachawene ameyasema hayo katika kiako kazi Cha wakuu wa idara za utawala na rasilimali watu katika utumishi wa imma kinachofanyika mkoa Arusha kwa siku tatu kikiwa na lengo la kujadili changamoto wanazokumbana nazo pamoja na kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi.

Hata hivyo mh waziri amesema kuwa usimamizi wa Rasilimaliwatu ni suala la msingi sana katika Taifa au Taasisi yoyote nchini, lengo kubwa likiwa ni kuongeza utendaji kazi wa Wafanyakazi na tija kwa Taasisi ili kufikia malengo ya kimkakati ya Taasisi.

"Mchakato wa usimamizi wa rasilimaliwatu huanza na muundo na uchambuzi wa ajira, ajira yenyewe, ulipaji wa mishahara, tathmini ya utendaji kazi mafunzo, motisha na stahiki mbali mbali za watumishi ,Pamoja na maeneo ya usimamizi wa Rasilimaliwatu kuainishwa, bado kumeendelea kuwa na Usimamizi wa Rasilimaliwatu usioridhisha katika Utumishi wa Umma hususani katika maeneo ya uzingatiaji wa Sera, Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo, maadili katika Utumishi wa Umma, matumizi yasiyoridhisha ya mifumo ya TEHAMA na kukosekana kwa uwajibikaji kwa baadhi ya Watumi,"

Aidha waziri amefafanua kuwa maadili ndio msingi katika utumishi wa imma na waachane na matumizi mabaya ya ofisi za umma,matumizi mabaya ya muda wa kazi, matumizi mabaya ya taarifa za ofisi.

"Niendelee kusisitiza umuhimu wa kuzingatia maadili kwa kuwa tumeendelea kupokea malalamiko kuhusu vitendo vya uvunjifu wa maadili ikiwemo Rushwa, lugha zisizofaa, kufanya udanganyifu wa nyaraka ikiwemo kughushi barua za masuala mbalimbali ya kiutumishi kama uhamisho wa kwenda sehemu zenye maslahi mazuri. "

Aidha mh waziri ameongeza kuwa ofisi yake imeendelea kupokea malalamiko ya watumishi waliostaafu kuhusu kucheleweshewa malipo ya mafao yao na hivyo amewaagiza kuhakikisha michango ya watumishi inawasilishwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa wakati na nyaraka zot zinazohitatajika ziandaliwe kwa wakati.

Kwa upande wake naibu katibu mkuu ofisi ya rais , menejimenti ya utumishi wa umma na utawala Bora Xavier mrope amesema kikao hiki kina lengo la kuendelea kuboresha utendaji kazi katika utumishi wa umma pamoja na kujadiliana mambo mbalimbali.

Xavier amesema kuwa kikao hiki kinauwezo wa kutoa na kupata taswira halisi ya usimamizi wa rasilimaliwatu katika utumishi wa umma na amesema bado Kuna changamoto mbalimbali za kiutendaji katika maswali ya kiutawala na usimamizi wa rasilimaliwatu katika utumishi wa umma .

Pia ameongeza kuwa changamoto hizo ndizo zinasababisha ucheweshaji wa kutoa huduma kwa wananchi au kutoa huduma kwa kiwango kisichoridhisha na hivyo husababisha mapungufu mengi ya kiutendaji ndani ya utumishi wa umma

No comments