Serikali inaimarisha Utekelezaji wa Dhana ya Afya Moja na utayari wa kukabiliana na dharura za kiafya” Dkt. Yonazi
Na Mwandishi wetu- Dodoma
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu imesema itaendelea kuratibu ushirikiano wa kisekta ndani na nje ya serikali kuhakikisha uimarishaji wa afya kwa umma ili kujenga uelewa kwa jamii kutambua kuwa suala la mapambano dhidi ya milipuko ya magonjwa ni la sekta zote.
Akizungumza wakati ufunguzi wa Kikao kazi cha Wadau cha Kuthibitisha Rasimu ya Taarifa ya tathmini ya Hali ya Utekelezaji wa Afya kwa wote na utayari wa kukabiliana na dharura Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Dkt. Jim Yonazi amesema kuwa kikao hicho ni moja kati ya juhudi za kuhakikisha Serikali na jamii yote inashirikishwa ipasavyo katika utekelezaji wa Afya kwa wote.
Dkt. Yonazi ameeleza kuwa tathmini hiyo inatoa fursa kwa nchi kuibua mapungufu kwa ajili ya maboresho na kubadilishana uzoefu na nchi nyingine hivyo kupitia Idara ya Menejimenti ya Maafa, Sehemu ya Afya Moja, Ofisi huunganisha wadau wote katika kushughulikia dharura za kiafya kwa binadamu, wanyama, mimea na mazingira.
“Kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya mwaka 2022 na Kanuni zake Ofisi huunganisha wadau wote katika kushughulikia dharura za kiafya. Aidha, Serikali ina miongozo, mikakati na taratibu za kiutendaji zinazowezesha utekelezaji, uwajibikaji na ushirikiano wa wadau ili kulinda afya ya binadamu, wanyama na mimea,”Amesema Dkt. Yonazi.
Pia ameishukuru sekretarieti ya wataalam kutoka Serikalini, mashirika ya Umoja wa Mataifa, Asasi za kiraia, Taasisi za utafiti na elimu kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kwa kutoa maoni yaliyowezesha kupata taarifa hiyo.
“Timu za wataalam kutoka sekta na wadau mbalimbali zimekuwa zikikutana kila wiki tangu Mwezi Agosti, 2023 kupitia nyaraka mbalimbali na kuandaa taarifa hii. Tathmini hii inatoa fursa kwa nchi kuibua mapungufu kwa ajili ya maboresho na kubadilishana uzoefu na nchi nyingine,” Amebainisha Katibu Mkuu huyo.
Aidha tathmini hiyo ni shirikishi na jumuishi ikiwa na lengo la kutambua maeneo ambayo nchi inafanya vizuri katika utekelezaji wa afya kwa wote na utayari wa kukabiliana na dharura.
Naye Afisa wa Masuala ya Dharura na Maafa kutoka Shirikia la Afya Duniani (WHO) Dkt. Faraja Msemwa amebainisha kwamba Tanzania ni Nchi ya Tatu Barani Afrika kuwa na mchakato wa Afya Moja ambao umeanza kutekelezwa mwaka 2022 kwa lengo la kuinua ajenda ya utayari wa kukabiliana na dharura kuhusu afya kwa wote pamoja na ushirikishwaji wa jamii nzima.
“Niipongeze Seraikli ya Tanzania kwa kuamua kulifanyia kazi hili kutokana na changamoto iliyowahi kuipata ikiwemo COVID-19 na homa ya Marburg pamoja na dharura ambazo si za afya moja na tunatoa rai kwa wadau wote wanaoratibu tushirikiane na Serikali tufikie lengo tunalokusudia,”Amesema Dkt. Msemwa.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akifungua kikao kazi cha Wadau cha Kuthibitisha Rasimu ya Taarifa ya Tathmini ya Hali ya Utekelezaji wa Afya kwa Wote na Utayari wa Kukabiliana na Dharura kilichofanyika Ukumbi wa Morena Dodoma tarehe 02 Novemba, 2023.
Afisa Masuala ya Dharura na Maafa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Faraja Msemwa akizungumza jambo wakati wa kikao kazi cha Wadau cha Kuthibitisha Rasimu ya Taarifa ya Tathmini ya Hali ya Utekelezaji wa Afya kwa Wote na Utayari wa Kukabiliana na Dharura kilichofanyika Ukumbi wa Morena Dodoma tarehe 02 Novemba, 2023.
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha Wadau cha Kuthibitisha Rasimu ya Taarifa ya Tathmini ya Hali ya Utekelezaji wa Afya kwa Wote na Utayari wa Kukabiliana na Dharura wakifuatili mawasilisho wakati wa kikao hicho.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Fatuma Toufiq wakati wa kikao kazi cha Wadau cha Kuthibitisha Rasimu ya Taarifa ya Tathmini ya Hali ya Utekelezaji wa Afya kwa Wote na Utayari wa Kukabiliana na Dharura.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Fatuma Toufiq akizungumza jambo wakati wa kikao kazi cha Wadau cha Kuthibitisha Rasimu ya Taarifa ya Tathmini ya Hali ya Utekelezaji wa Afya kwa Wote na Utayari wa Kukabiliana na Dharura.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Charles Msangi akifafanua jambo wakati wa kikao hicho.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (wa tatu kutoka kushoto waliokaa) pamoja na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao kazi cha Wadau cha Kuthibitisha Rasimu ya Taarifa ya Tathmini ya Hali ya Utekelezaji wa Afya kwa Wote na Utayari wa Kukabiliana na Dharura.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Post a Comment