Header Ads

test

Mkurugenzi wa Kanda: Wahitimu wenye ujuzi hawatembei na bahasha za maombi ya kazi

Asema kazi zao ziko mikononi mwao sio bahasha 

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV


MKURUGENZI wa VETA Kanda ya Dar es Salaam , Angelus  Ngonyani  amesema kuwa VETA ndi nguvu kazi katika maendeleo kutokana ujuzi wanaotokana nao katika vyuo.

Wahitimu wenye ujuzi hawawezi kutembea na bahasha kwa ajili ya kutafuta  ajira kutokana wao ujuzi wao ndio unahitajika katika sehemu nyingi na sio bahasha.

Ngonyani ameyasema hayo kwenya mahafali ya 12 ya Chuo VETA KiKauli hiyo aliitoa jijini Kipawa yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho Dar es Salaam.

Amesema kuwa vijana wanaohitimu VETA wana fursa ya kujiajiri pamoja na kuajiriwa hivyo ni kazi yao kwenda kuonyesha umahiri katika maeneo waliyosomea.

Amesema ana  katika mahafali ya wahitimu wa kozi ya Tehama ndio dunia ilipo sasa viwanda vinatumia mifumo ambayo kazi yenu  kwenda kusimamia.

Amesema kuwa katika Chuo hicho kozi wameongeza kozi ya viwanda vya vinywaji mbalimbali kwa kusoma kwa vitendo na vifaa vya kufundishia vinajitosheleza.

Amesema kuwa katika awamu ya sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameleta mafanikio katika vyuo kwa kujenga miundombinu pamoja na vifaa vya kisasa.

Ngonyani amesema kuwa kazi ya Mhandisi mmoja anahitaji kuwa na mafundi 25 ambao hao wanazalishwa na vyuo vya VETA.

"Katika zama za sasa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na Dunia ndiko iliko sasa kwa VETA Kipawa ina Deni ya kuzalisha wahitimu wa kutosha wa kuhudumia teknolojia hiyo" amesema Ngonyan

Amesema serikali inaendeleea na upanuzi wa Chuo hicho  kuhakikisha utoaji wa huduma za ufundi stadi zinaongezeka na Mkoa wa Dar es Salaam kuna jumla ya vyuo viwili na mkakati uliopo ni kuongeza vitatu ili kukidhi mahitaji ya soko yanayoonekanaa kutokana na serikali kufungua uwekezaji wa viwanda na shughuli zingine za kiuchumi.

Pia alisema uwepo wa Chuo hicho katika eneo la Kipawa ni mkakati uliojikita kutoa mafunzo katika mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hivyo wahitimu 32 waliomaliza wapo  katika hatua nzuri ya kupata ajira za uhakika.

Ngonyani amesema  katika mapinduzi ya nne ya Tehama teknolojia ndio hutumika hivyo kupitia chuo hicho anatarajia watapiga hatua kwa kutoa vijana wa uhakika katika kuleta maendeleo ya mapinduzi ya Viwanda.

Hata hivyo aliwataka wahitimu hao ku wabunifu na kuja na mfumo wa kuchakata taka Kwa kutumia teknolojia.

Kwa upande wake ,Mkuu wa Chuo cha Tehema VETA Kipawa, Mhandisi Sospeter Mkasanga  amesema tangu kuanzishwa kwake, jumla ya wanafunzi 9752 wamefanikiwa kupata mafunzo katika Chuo hicho na wanaendelea kufanya kazi mbalimbali.

Amesema chuo hicho ni miongoni mwa vyuo mahiri katika mafunzo ya Tehama hivyo amewata viongozi mbalimbali kuongeza ujuzi kupitia chuo hicho kukuza uchumi wa kidigitali.
 
Pia aliwashauri wahitimu  wasiridhike na elimu waliyonayo bali wajiendeleze kuendana na soko la ajira nchini.

Akisoma  risala Kulwa  James alisema wahitimu hao wapo tayari kujenga taifa lao kwa kadri ya ujuzi walioupata na kuwa mabalozi wa kutangaza chuo hicho.

Alisema kwa mfano ujuzi wa umeme utawasaidia kuweka mifumo ya umeme hasa maeneo ya nyumbani hivyo kushirikiana na serikali kuondoa hitilafu mbalimbali.

Hata hivyo aliishauri serikali kuziagiza taasisi za umma na binafsi kutoa ajira  kwa lengo la kuwasaidia wahitimu wengi.

Kwa upande wa Mwajiri Mwakilishi wa Meneja wa Tanesco Adrian Severin amesema wahitimu wasibwete na elimu walioipata bali waendelee kusoma katika kujipa maarifa zaidi.

Amesema kuwa wale walisoma umeme wajisajiri EWURA na kupata leseni ambapo wanaweza kufanya kazi za umeme majumbani.

Kwa upande wa Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama Erick Mkuti amesema serikali inaendelea kuimarisha kwa huduma za Tehama nchini.Mwanafunzi akionesha umahiri wa ujuzi katika maonesho wahitimu chuo cha VETA Kipawa kwenye Mahafali ya 12 jijini Dar es Salaam.Meza kuu katika mahafali ya VETA wakipata elimu kuhusiana na ufundi simu wa kisasa unaotumia vifaa vya kisasa kutoka kwa wahitmu wa Chuo cha VETA Kipawa kwenye mahafali 12 yaliyoambatana na maoneshoMwanafunzi na Mhitimu akionesha umahiri wa ujuzi katika maonesho wahitimu chuo cha VETA Kipawa kwenye Mahafali ya 12 jijini Dar es Salaam.

Mhitmu Dorice Tesha akionesha mfumo wa viwanda vya vinywaji vinavyoweza kuendesha shughuli za uzalishaji wakati Meza kuu ilipotembelea moja ya darasa katika mahafali ya 12 Chuo cha VETA Kipawa.
Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam Angelus Ngonyani akizungumza katika mahafali ya 12 ya Chuo Cha Tehama VETA Kipawa yaliyofanyika kwenye chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Tehama VETA Kipawa Mhandisi Sospeter Mkasanga akitoa maelezo kuhusiana mafunzo yanayotolewa na Chuo cha VETA  Tehama  Kipawa  kwenye  mahafali 12 jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Meneja wa Tanesco  kwa upande wa waajiri Adrian Severin akizungumza kuhusiana na mafunzo waliopata na fursa katika soko la umeme katika mahafali 12 Chuo cha Tehama VETA  Kipawa jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama Erick Mkuti  akizungumza kuhusiana na mafunzo waliopata na fursa zilizopo kwenye dunia ya Tehama katika  mahafali 12 Chuo cha Tehama VETA  Kipawa jijini Dar es Salaam.

No comments