Operesheni ya TMDA yabaini uchepushaji wa Dawa za Serikali
Majalada 13 Mahakamani kwa ajili ya Kesi kwa wahusika
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
Wizara ya Afya kupitia Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais,Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA),Baraza la Famasi ,Tamisemi pamoja na Jeshi la Polisi iliendesha operesheni ya ukaguzi na kubaini kuwepo kwa dawa za serikali zilizochepushwa katika vituo binafsi.
Dawa za Serikali zilizokutwa katika katika maduka ya dawa binafsi ni Dawa za Malaria Mseto ya Vidonge aina ya ALU ,Dawa ya Mseto ya kutibu Kifua Kikuu na Dawa za Uzazi wa mpango ambapo dawa hizo ziikutwa katika maduka kwenye mikoa ya Dar es Salaam,Lindi ,Ruvuma pamoja na Simiyu.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Adam Fimbo amesema kuwa Operesheni hiyo ilifanyika kati ya Novemba 20hadi24 Novemba Mwaka huu lengo ni kutaka kuwa wanahusika na mnyororo wa dawa kuendelea kuwa bora katika kulinda afya ya wananchi.
Amesema operesheni hio ililenga kufanya ukakugazi na msako mkali wa bidhaa za afya kwenye hospitali, vituo yva afya, zahanat,maghala,maduka ya jumla na lejaleja ya watu binafsi na mengine yasiyo rasimi.
Amesema operesheni hiyo ilifanyika katika Wilaya katika Mikoa 13 ya Dar es Salaam,Dodoma ,Morogoro ,Kigoma,Katavi Mwanza,Simiyu ,Arusha ,Kilimanjaro ,Mbeya,Songwe,Lindi pamoja na Ruvuma.
Fimbo amesema Wilaya zzilizochaguliwa zilitokana na kuwa na rekodi za matokeo miaka ya nyuma ya ukaguzi mbalimbali za TMDA pamoja na taarifa za Kiintelejensia kutoka katika vyombo vya udhibiti.
Amesema maeneo yaliyokaguliwa ni Majengo 777ambapo Famasi 283,Maduka 23 ya Vifaa tiba ,Maghala Tisa ya Dawa,Maghala Mawili ya Vifaa tiba,Maduka 105 ya Dawa ya Mifugo,Maduka 272 ya Dawa Muhimu za Binadamu (DLDM),vituo 30 vya kutolea huduma za Afya katika Hospitali ,Zahanati,Vituo vya Afya na Kiliniki ,Maabara 32 na Kiwanda Kimoja cha Dawa.
Amesema casa zilizoisha matumizi zenye inayokadiriwa sh.10,313,960 zilikamatwa na dawa hizo zilikuwa hazijatengewa kwa mujibu wa utaratibu na sehmu kubwa ya vifaa tiba vilikamatwa Kanda ya Mashariki ,Kanda ya Ziwa Mashariki na Nyanda za Juu Kusini
Amesema majalada 13 yamefunguliwa na yako Mahakamani na faini 100 zilozohusiana na makosa yaliyopo kwa mujibu wa sheria.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Adam Fimbo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Operesheni iliyofanywa na TMDA kwa kushirikiana na taasisi zingine za Udhibiti jijini Dar es Salaam.
Post a Comment