MAKAMU MWENYEKITI INEC ATEMBELEA MAFUNZO YA WAENDESHA BVR PEMBA
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk (kushoto) akimsikiliza Afisa wa Tume kutoka Idara ya TEHAMA na Daftari, Lazaro Madembwe aliyekua akimpa ufafanuzi wakati alipotembelea kituo cha mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki katika Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo Oktoba 5, 2024 katika siku ya pili ya mafunzo hayo. Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni maandalizi ya mzunguko wa sita wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao utajumuisha mikoa mitano ya Zanzibar ambapo Uboreshaji wa Daftari kwenye maeneo hayo utaanza Oktoba 07 hadi Oktoba 13, 2024 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni. (Picha na INEC).
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk (kulia) akifurahia jambo wakati alipotembelea kituo cha mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki katika Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba leo Oktoba 5, 2024 katika siku ya pili ya mafunzo hayo. Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni maandalizi ya mzunguko wa sita wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao utajumuisha mikoa mitano ya Zanzibar ambapo Uboreshaji wa Daftari kwenye maeneo hayo utaanza Oktoba 07 hadi Oktoba 13, 2024 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni. (Picha na INEC).
Post a Comment