WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzani (TFS) umewataka watanzania kuchangamkia fursa ya Utalii wa Nyuki
WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzani (TFS) umewataka watanzania kuchangamkia fursa ya Utalii wa Nyuki, kutumia sumu ya nyuki kama tiba mbadala ya magonjwa mbalimbali ya kuambukizwa na yasiyoambukizwa.
Mhifadhi Mwandamizi wa TFS kutoka Shamba la Miti Silayo, Juma Mdoe amefafanua hayo wakati akitoa elimu mbele ya wananchi katika Maonesho ya Saba ya Teknolojia ya Madini mjini Geita.
Alisema tafiti zinaonesha kuwa sumu ya nyuki ina mchanganyiko wa kampaundi nyingi zilizotengenezwa na nyuki ambapo mwilini mwa binadamu inasaidia kumkinga na vimelea vya magonjwa mbalimbali.
Lisa Richard mkazi wa Mkoa wa Geita ambaye anafanya kazi Benki ya CRDB amesema hii ni mara ya 3 kufika Banda la Maliasili na kutumia Tiba hiyo ya kudungwa na Nyuki na amesema kwake inamsaidia kujikinga na maradhi na baada ya kutumia njia hiyo ya Tiba ya Nyuki atakuwa anafanya mara kwa mara peke yake kwa kuzingatia maelekezo ya wataalam wa ufugaji nyuki kwa kuwa elimu hiyo imemsaidia baada ya kufika katika Banda la Maliasili.
Post a Comment