MAMIA WAJITOKEZA HUDUMA ZA UCHUNGUZI WA MACHO HOSPITALI YA MBAGALA
Mamia ya wakazi wa Mbagala iliyopo Manispaa ya Temeke, Jijini Dar es Slaam, jana wamejitokeza kwa wingi Hospitali ya Mbagala Rangi Tatu ili kufanyiwa uchunguzi wa macho unaofanywa na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) bila malipo kwa kushirikiana na wenzao hospitalini hapo.
Akizunguma hospitalini hapo, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dkt. Jonas Lulandala, amewataka wananchi kujitokeza kutumia fursa hiyo ya upimaji macho bila malipo ulioratibiwa na Manispaa ya Temeke kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo watakaogundulika na changamoto kubwa zinazohitaji upasuaji watapata huduma hiyo kupitia upasuaji wa tundu dogo utakaofanyika MNH.
Sambamba na hilo, Dkt. Lulandala ameushukuru Uongozi wa MNH na watoa huduma kutoka hospitalini hapo kwenda kutoa huduma katika maeneo walipo wananchi ambapo hadi jana majira ya saa tano zaidi ya wananchi 300 walikua wamejiandikisha kupata huduma hiyo itakayohitimishwa tarehe 29 Novemba, 2024.
Post a Comment