MARAIS wa Nchi Nane za EAC Kuhudhuria Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 25 ya EAC.
Na Jane Edward, Arusha
Marais wa nchi nane za Jumuiya ya Afrika Mashariki wanatarajia kukutana jijini Arusha kuanzia Novemba 29 kwaajili ya kushiriki Vikao vya kawaida pamoja na kuongoza Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Arusha Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bi Veroniva Nduva ameeleza kuwa maandalizi ya Maadhimisho ya Miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanaenda sambamba na kutoa elimu kwa wananchi juu ya shughuli zinazofanywa na jumuiya hiyo.
Akizungumzia ratiba za Maadhimisho hayo ya Miaka 25 ya Jumuiya ya afrika Mashariki yatakayofanyika Kwenye kituo cha Kimataifa cha Mikutano AICC Jijini Arusha, Bi Nduva ameeleza kuwa kutakuwa na Tamasha la Kitamaduni litakalojumuisha Washiriki kutoka nchi zote za EAC,huku Vikao mbalimbali vikijadili kuhusu Amani na Usalama kwa EAC pamoja na Changamoto na mafanikio ya Jumuiya hiyo.
Post a Comment