Header Ads

test

WANAWAKE WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA

 

Na Mwandishi Wetu Michuzi TV 

KAIMU Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala, Tabu Shaibu, amewashauri wanawake wote kuchangamkia fursa zinazojitokeza ili ziwasaidie kujiinua kiuchumi na kuepuka kuwa tegemezi

Ushauri huo umetolewa leo Novemba 1,2024 Jijini Dar es salaam wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa bajaji inayotumia nishati ya umeme wa jua( Solar) kwa wanawake wanufaika wa mradi wa 'She drive to change' waliopatiwa mafunzo ya udereva kwa ufadhili kutoka Ujerumani 

" Niwapongeze sana shirika la Ladies Joint Forum( NGO),  kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Ujerumani kuweza kuwafundisha wanawake 30 udereva na wote na kuwapatia leseni  huku mkiangalia namna ya kuwapatia vyombo vya usafiri ili waweze kujiinua kiuchumi mimi naamini mwanamke ndiye mwangalizi wa familia akiwezeshwa anaweza kuinua na wengine" amesema Tabu

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Ladie Joint Forum Francisca Mboya amesema bajaji hiyo iliyozinduliwa  wanufaika wa mradi wa She dreve to change ambapo watajipatia kipato na wataendelea kuongeza bajaji nyingine kupitia fedha mbalimbali watakazochangiwa na wadau.

" She drive to change ni mradi wa  miezi 12 uliolenga  kuwezesha na kukuza.uhuru wa kiuchumi wa wanawake 30 wenye umri wa miaka 18-40 katika kata ya Vingunguti Wilaya ya Ilala Jijini Dar es salaam na unazingatia hasa wahanga walionyanyaswa kijinsia,kina mama vijana walemavu na wale wanaolea watoto wenye ulemavu peke yao" amesema Francisca

Kwa upande wake Mnufaika wa mradi huo Oliva Mushi amesema yeye amemudu familia kwa kulipia ada ya shule watoto wake , anajitegemea kwani hapo awali alikuwa anaishi wa ndugu ila tangu amepatiwa leseni anaendesha bajaji na amewashauri wanawame wengine wasikate tamaa ya  mafanikio kwani hayapatikani kwa siku moja.




 

No comments