WAZIRI BITEKO KUFUNGUA MKUTANO MKUU WA SABA WA JUMUIYA MAMLAKA ZA USIMAMIZI WA USAFIRI MAJI AFRIKA
Na Lilian Ekonga. Dar es salaam.
Tanzania kupitia shirika la uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imeteuliwa kuwa nchi mwenyeji kwenye wa Makutano wa saba (7) wa akimataifa wa jumuiya ya Mamlaka za usimamizi wa usafiri Majini Barani Afrika utakaofanyika kuanzia tarehe 29 novemba hadi 10 Disemba 2024 jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema lengo la mkutano huo ni kujadili masuala muhimu ya maendeleao ya udhibiti na usimamizi wa usalama wa usafiri majini hatani afrika.
Amesema kipaumbele kikiwa ni mustakabali wa usafiri wa majini ma kuongeza ushirikiano baina ya nchi na wanachama.
"Kauli mbiu ya mkutano huo ni ' Kuimarisha mustakabali wa sekta ya usafiri majini barani Afrika, ushirikianao katika teknolojia na ubunifu ili kupunguza hewa ukaa, kuimarisha usalama wa mazingira, na mazingira ya sekta ya usafiri majini kwa mustakabali endelevy"amesema
Ameongeza kuwa mkutano utafunguliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Dotto Biteko na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa shirika la Bahari Duniani, Bw Antonio Dominguez pamoja na wataalam wa usafiri majini, viongozi wa mamlaka za udhibiti wa usafiri kutoka nchi na wanachama wa umoja wa Afrika zipatazo 50 ambazo zina bahari.
Pia Waziri amesema mkutano huo utatatumika kama jukwaa muhimu katika kuwezesha wadau kushiriki katika majadiliano yanayogusa masuala ya teknolojia na ubunifu yenye kulenga katika kuimarisha usalama wa usafiri majini.
"Ushiriki wa Bw. Dominguez ni heshima kubwa kwa Tanzania hasa kipindi hiki tunapotekeleza sera ya Taifa ya uchumi wa Buluu ambapo kama nchi tumebainisha masuala ambayo serikali kwa kushirikiana na Wadau" amesema waziri Biteko
Aidha amebainisha Tanzania itaendelea kutangaza fursa za kiuchumi zilizopi katika sekta ya usafiri kwa njia ya maji zinazohusiana na utumiaji wa rasilimali za habari na maziwa zitakazo saidia kuongeza uwezo wa serikali kuwa hudumia wananchin na kuwaletea maendeleo.
Alikalika ametoa wito kwa wadau wa sekta ya usafiri majini, wakiwemo wasafirishaji, wamiliki wa vyombo vya usafirishaji majini, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, viongozi wa serikali kujitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano huo muhimu.
Post a Comment