AIRTEL AFRICA YAJIVUNIA MAFANIKIO ROBO YA KWANZA 2025
Na Mwandishi Wetu
AIRTEL Africa imetangaza matokeo bora kwa robo ya kwanza iliyoishia Juni 30, 2025, ikionesha ongezeko la wateja wanaotumia huduma za intaneti na Airtel Money katika nchi mbalimbali baranı Afrika.Alizungumza leo jijini Dar es Salaam Ofisa Mtendaji Mkuu, Sunil Taldar, amesema kwamba mafanikio ambayo wameyapata ni matokeo ya utekelezaji wa mkakati thabiti unaolenga kuboresha huduma kwa wateja na kuwekeza katika teknolojia mpya ikiwemo Airtel Spam Alert ili kuhakikisha usalama na kuimarisha imani ya mtandao.
Amesisitiza kuwa wataendelea kukuza ujumuishaji wa kifedha na kuunganisha jamii nyingi zaidi barani Afrika na kuonngeza Airtel Africa imeshukuru wafanyakazi na wadau wote kwa mchango wao katika kuhakikisha ukuaji endelevu na huduma bora kwa wateja nchini Tanzania na kwingineko.
“Hakika matokeo haya ya mafanikio ambayo tumeendelea kuyapata tunawashukuru wadau wote kwa mchango ambao umetuwezesha katika kuwa na mafanikio ya ukuaji huu endelevu katika kutoa huduma bora kwa wateja wetu.”
Post a Comment