Posta Yasisitiza Mchango Wake kwa Wakulima Kupitia Usafirishaji wa Pembejeo na Bidhaa
Shirika la Posta Tanzania limesisitiza dhamira yake ya kusaidia maendeleo ya kilimo nchini kwa kusafirisha pembejeo, mbegu, na bidhaa mbalimbali kutoka kwa wauzaji hadi kwa wakulima katika maeneo yote ya Tanzania kwa gharama nafuu.
Ikishiriki katika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, Shirika hilo limeeleza kuwa linachukua nafasi muhimu kama kiunganishi kati ya wazalishaji na walaji, kwa kuhakikisha bidhaa na huduma muhimu zinafika kwa wakati na kwa usalama.
Katika maonesho ya mwaka huu, Posta inatoa huduma maalum ya kusafirisha mizigo ya wateja kutoka viwanjani hadi majumbani kwa kutumia bajaji maalum, huduma ambayo imepokelewa kwa mwitikio chanya kutoka kwa wananchi.
Huduma nyingine zinazopatikana katika banda la Posta ni pamoja na usajili wa huduma ya EMS, ufunguaji wa masanduku ya barua, malipo ya ada za masanduku pamoja na usajili wa huduma ya kisasa ya VIRTUAL BOX kwa urahisi.
Posta inatoa wito kwa wananchi wanaotembelea maonesho hayo kutembelea banda lake ili kupata elimu na huduma bora zinazolenga kurahisisha maisha na biashara zao.
Post a Comment