SERIKALI YAWEZESHA HUDUMA ZA POSTA KIDIJITALI KUPITIA VIFAA VYA TEHAMA KUTOKA UCSAF
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa, amesema Serikali ya Awamu ya Sita imejipanga kuhakikisha huduma za msingi ikiwemo Posta, Mawasiliano, intaneti na huduma za kifedha za kidijitali zinawafikia wananchi wote bila kujali jiografia.
Waziri Silaa aliyasema hayo jijini Dar es Salaam, Agosti 22, 2025, katika hafla ya makabidhiano ya vifaa vya kisasa vya TEHAMA kutoka Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwenda Shirika la Posta Tanzania.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mtendaji Mkuu wa UCSAF alibainisha kuwa makabidhiano hayo ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha huduma za mawasiliano na kidijitali, hususan maeneo ya pembezoni, ili kuongeza kasi, ufanisi na ubunifu wa huduma za Posta na kulifanya Shirika la Posta kuwa daraja la biashara mtandaoni kwa Watanzania wote.
Kwa upande wake, Postamasta Mkuu, Bw. Macrice Daniel Mbodo, aliishukuru UCSAF kwa ushirikiano thabiti na kusisitiza kuwa vifaa hivyo vitasambazwa mara moja katika mikoa yote ya Posta nchini ili wananchi waanze kunufaika.
Aliongeza kuwa hatua hiyo itaboresha kasi ya huduma, kuongeza uwazi na kurahisisha upatikanaji wa huduma za Posta kupitia mifumo ya kisasa.
Post a Comment