Header Ads

test

Mhe. Mchengerwa afungua kikao cha Mawaziri wa Afrika wa Afya kuhusu kampeni ya kupunguza vifo vya mama na mtoto (CARMMA) kwa niaba ya Rais Samia

Azitaka nchi za Afrika kuunganisha nguvu

Wajumbe wamsifu Rais Samia kwa kuwa kinara

Na John Mapepele- Addis Abbaba. 

Waziri wa afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa  amesema Afrika inatakiwa kuunganisha nguvu katika kuweka mikakati ya pamoja  katika kupunguza  vifo vya mama  na mtoto ili kuondokana na  changamoto  hiyo.

Mhe. Mchengerwa ametoa kauli hiyo leo Februari 13, 2026 jijini Addis Abbaba nchinini Ethiopia   kwenye  mkutano wa Nchi zote za Umoja wa Afrika wakati anafungukua mkutano huo, akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Mchengerwa amesema Umoja wan chi za Afrika umeipa Tanzania heshima kubwa  ya kufungua mkutano huo kwa kutambua juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Tanzania ikiongozwa na Rais, Samia Suluhu Hassan  katika kupunguza kwa kasi vifo  vya mama na mtoto  wakati wa kujifungua.

“Ni ukweli usiopingika kuwa Rais Samia amefanya kazi kubwa sana  katika eneo hili la kupunguza  vifo vya mama na mtoto katika kipindi kifupi na kupata tuzo nyingi, na  ndiyo sababu wameipatia nchi yetu hesghima  ya kufungua  mkutano huu mkubwa”.Amefafanua Mhe. Mchengerwa

Mkutano  huu umehudhuliwa  na takribani nchi zote za Afrika ambapo mawazari wa Afya wa nchi hizo wamepata fursa ya kufanya majadiliano ya namna bora  ya kukabiliana na  changamoto ya vifo vya mama na mtoto huku Tanzania ikipigiwa mfano wa kufanya vizuri katika eneo hili.

Aidha, wajumbe  wameonyesha kuridhishwa na hatua zinazochukuliwa  na nchi  wanachama  na kwamba kumekuwa na mafanikio yanayoonekana kupitia kampeni ijulikanayo kama CARMMA (2021- 20300 chini ya Umoja wa Nchi za Afrika inayolenga  kupunguza  vifo  vya mama na mtoto.

Mkutano huu unafanyika jijini Addis Ababa nchini Ethiopia pembezoni mwa Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika unaofanyika kesho na kesho kutwa ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anashiriki na amependekezwa kuwa kinara wa Umoja wa Afrika katika Masuala ya   Afya ya Mama na Mtoto, uteuzi ambao unatarajiwa kupitishwa rasmi na Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali.


 

No comments