Header Ads

test

VIFAA TIBA VYA KISASA VILIVYOTOLEWA NA MSD VYANOGESHA HUDUMA MATIBABU HOSPOTALI YA JIJI LA DODOMA

Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Dodoma

WAKAZI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameendelea kupata huduma bora za afya katika Hospitali ya Jiji huku Bohari ya Dawa(MSD)ikiwezesha utolewaji wa huduma hizo kupitia vifaa tiba vya kisasa na dawa zote muhimu ilivyopeleka hospitalini hapo.
Kuanza kwa huduma kwa Hospitali hiyo imewezesha wakazi  wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wapato 765,179 wakiwemo wanaume 373,440 na wanawake 391,739 kufurahia matunda ya hitaji ya sera ya mwaka 2009 ya kusogeza huduma karibu na wananchi ,hivyo kupitia fedha za halmashauri  na Serikali kuu ujenzi ulianza na sasa wananchi wanapata huduma za matibabu kwa raha mustarehe.

Kupitia ziara iliyoandaliwa na MSD kwa wahariri na waandishi wa habari Mganga Mfawindhi wa Hospitali ya Dodoma Dk.Joshua Mwalongo amesema hadi sasa jumla ya fedha ambazo zimepelekwa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo ni Sh.bilioni 2.8.

Kwa mujibu wa Dk.Mwalongo hospitali hiyo imekuwa na manufaa makubwa hasa ya kusogeza huduma za matibabu karibu na wananchi na tangu ilipoanza kutoa huduma Januari 20,2025 wananchi wameendelea kuongezeka siku hadi siku huku akisisitiza MSD imewezesha vifaa tiba vya kisasa kwa ajili ya matibabu mbalimbali.

Akifafanua kuhusu mradi huo amesema ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ulitokana na uhitaji wa wanachi kupata huduma za ngazi ya hospitali ya wilaya na hiyo ni kutokana na changamoto ya kukosa Hospitali ya Wilaya kwa muda mrefu.
“Pia ujenzi ulitokana na hitaji la sera ya Afya ya mwaka 2009 la kusogeza huduma karibu na wananchi hivyo kupitia fedha za Halmashauri na Serikali kuu, ujenzi wa hospitali hii ya Wilaya ulianza rasmi mnamo mwaka 2023,”amesema na kuongeza shilingi 100,000,000.00 zimetumika kununua vifaa tiba kutoka Bohari ya Dawa MSD.

Akieleza zaidi amesema hospitali hiyo hadi sasa ina majengo 10 ya kutolea huduma , na kuomgeza kwa mwezi wanahudumia wagonjwa 700

Katika kutambua mchango wa Serikali katika ujenzi wa hospitali hiyo Dk.Mwalongo amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa hospitali hiyo ambayo imepunguza msongamano katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na Hospitali ya Makole.

“Wananchi hawaendi huko wanakuja katika hospitali ya Wilaya na kwa kweli tunaishukuru MSD kwa kutuwezesha vifaa tiba vya kisasa pamoja na dawa zote muhimu ambazo tunazipata kwa wakati.Upatikanaji dawa kwetu ni zaidi ya asilimia 93.”

Awali Meneja MSD kanda ya Dodoma Mwanashehe Jumaa amesema uwepo wa hospitali hiyo sambamba na na vifaa tiba vinavyosambazwa MSD itasaidia kutoka huduma za uhakika na kupunguza msomgamano katika hospitali nyingine huku akiwahakikishia watanzania MSD itaendelea kupeleka Dawa na vifaa tiba vya kisasa kwa wakati.

Pamoja na hayo jambo la kufurahisha zaidi hospitali hiyo kuanza kutoa huduma za matibabu kwa magonjwa mbalimbali pia imefungua fursa ya ajira kwa vijana wa kitanzania kwani idadi kubwa ya watoa huduma katika hospitali hiyo ni vijana zaidi ambao hivi sasa wanaenjoi kutoa huduma kwa vifaa tiba vya kisasa.Madaktari wanabofya tu.







 

No comments