CHONGOLO AKWAMUA UJENZI WA ZAHANATI ULIOKWAMA KWA ZAIDI MIAKA 10
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo amekwamua ujenzi wa Zahanati ya Kinambeu iliyopo Iramba mkoani Singida iliyokwama kwa zaidi ya miaka 10 kwa kuagiza Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuhakikisha inapeleka fedha haraka ili kikamilike na kuwaondolea adha wananchi ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.
Chongolo ametoa maelekezo hayo tarehe 01 Machi, 2023 alipotembelea na kukagua majengo ya zahanati hiyo ambayo yaliyanza kujengwa mwaka 2011.
Akiwa hapo Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo baada ya kupokea Ripoti ya Ujenzi wa Zahanati hiyo, ameitaka TAMISEMI na Halmashuri ya Iramba kuhakikisha zahanati hiyo inakamilika haraka iwezekanavyo ili wananchi waondokane na adha ya kukosa huduma za afya.
Zahanati hiyo ujenzi wake hadi sasa umegharimu Shilingi Milioni 185.9 ambapo Mhisani kutoka Japan alitoa Shilingi Milioni 158.8, Halmashauri Shilingi ya Iramba Milioni 20.04 na jamii kutoa nguvu kazi zenye Gharama ya Shilingi Milioni 7.06 na mkandarasi aliishia kukamilisha kazi ya Ujenzi wa kuta na kupaua Desemba mwaka 2015.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo anaendelea na ziara yake Mkoano Singida akiwa ameambatana na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa itikadi na Uenezi Ndugu sophia Mjema pamoja na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Oganaizesheni Issa Haji Gavu
Post a Comment